tangazo

VW yaamuriwa kulipa fidia kashfa ya 'dieselgate'

Mahakama ya juu ya kiraia nchini Ujerumani imehukumu dhidi ya Volkswagen, katika kesi ya kwanza iliyofunguliwa na mmiliki wa gari dhidi ya kampuni hiyo ya magari kuhusu udanganyifu wa vipimo vya uchafuzi wa mazingira.
Mahakama kuu ya kiraia nchini Ujerumani imepitisha uamuzi dhidi ya kampuni ya Magari ya Volkswagen katika kesi ya kwanza iliyowasilishwa na mtumiaji gari ya kampuni hiyo kufuatia suala zima la udanganyifu wa vipimo vya kiwango cha moshi unaotoka kwenye magari. Uamuzi huu umefungua njia kwa maelfu ya kesi nyingine zaidi kuelekea kampuni hiyo.
Mahakama ya haki ya shirikisho siku ya Jumatatu 25.05.2020 imepitisha uamuzi dhidi ya kampuni hiyo ya Kijerumani ya Volkswagen katika kesi ya kwanza nchini humo iliyofunguliwa na mmiliki mmoja wa gari ya kampuni hiyo.
Mahakama imesema kwamba watu walionunua magari ya Volkwagen yaliyowekwa programu maalum ambayo inachezea vipimo vya kiwango cha moshi wa gari wanastahili kulipwa fidia ya kifedha.

Mwakilishi wa upande wa utetezi Herbert Gilbert akiwa katika chumba cha mahakama wakati majaji wakiwasili kwa ajili ya kutoa hukumu yao katika kesi dhidi ya Volkswagenm Mei 25, 2020.

Watu hao wanaweza kuyarudisha magari na kurudishiwa kiwango fulani cha fedha kutoka kampuni hiyo. Aidha katika utaratibu uliopo kiwango cha kilomita zilizotumika kitazingatiwa wakati wa wateja hao kuhesabiwa fidia yao kwa mujibu wa uamuzi wa mahakama hiyo.

Post a Comment

0 Comments