tangazo

Wachina 4 wakamatwa kwa kuhifadhi Sarafu za Mil 200

Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Morogoro, imekamata watu wanne raia wa China kwa kosa la kuhifadhi fedha, ambazo ni Sarafu za Tanzania zaidi ya Shilingi Milioni 200, kinyume na sheria katika nyumba moja iliyopo Mtaa wa Mwere Manispaa ya Morogoro.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo, amesema kuwa awali walipata taarifa kutoka kwa baadhi ya wananchi wakiwatilia shaka raia hao wa China, baada ya kuona wakiingia na kutoka katika nyumba hiyo ndipo walipoamua kuchukua hatua ya kuwafuatilia na kubaini wanamiliki kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Bonanza.

"Kwa kawaida hizi pesa hata kama unafanya biashara zinatakiwa ziende Benki, lakini wao wamezihodhi ndani ya nyumba, na tulipofanya msako tumekuta kuna viroba vimejaa pesa na kwenye mashine na spare parts zake ni pesa za Kitanzania awali walituambia ziko Milioni 2, lakini tumegundua zipo zaidi ya Milioni 200 ambazo ni Sarafu" amesema DC Chonjo.

Aidha DC Chonjo amesema kuwa hatua zilizopo kwa sasa, watawafungulia mashtaka kwa kosa la kuhodhi pesa ambazo hazipo kwenye mzunguko kinyume cha sheria.

Post a Comment

0 Comments