tangazo

Wafungwa takriban 10,000 waachiwa huru ufilipino

Hakimu wa mahakama kuu nchini Ufilipino amesema takriban wafungwa 10,000 wameachiwa huru wakati taifa hilo likijitahidi kudhibiti virusi vya corona katika magereza yake yaliojaa wafungwa.

Hatua hii inafuatia maagizo yaliotolewa ya kuwaachia huru wafungwa wanaosubiri kushitakiwa kwasababu hawakuweza kulipa dhamana, alisema hakimu huyo Mario Victor Leonen alipozungumza na waandishi habari.

 Msongamano katika magereza nchini Ufilipino ni tatizo kubwa tangu rais Rodrigo Durtete alipoanzisha hatua za kuwafuatilia wafanyabiashara ya madawa ya kulevya mwaka 2016.

Ugonjwa wa COVID 19 umeripotiwa katika baadhi ya magereza yaliojaa watu na kuwaathiri wafungwa pamoja na maafisa wa magereza nchini Ufilipino.

 Kulingana na mfumo wa magereza nchini humo kukaa umbali wa mita moja na nusu kati ya mtu na mtu ni jambo lisilowezekana kufuatia wafungwa kurundikana mara tano ya kiwango kinachohitajika katika chumba kimoja cha magereza nchini humo.

Post a Comment

0 Comments