Walinzi wa amani 500 wapelekwa Minnesota na St. Paul


Wanajeshi 500 wa kikosi cha ulinzi wa taifa pamoja na wanajeshi wa anga wamesambazwa kwenye miji ya kaskazini mwa Marekani ya Minnesota na St. Paul baada ya siku tatu za maandamano ya vurugu, kufuatia kifo cha mmarekani mweusi George Floyd.

Meja Jenerali wa jeshi Jon Jensen wa kikosi cha walinzi hao cha Minnesota amesema wanajeshi waliosambazwa wana mafunzo ya kuwalinda raia, mali na kuhakikisha haki ya watu kuandamana kwa amani.

Hatua hiyo ilianza usiku wakati waandamanaji walipoanza kupora na kuchoma majengo kadhaa kote kwenye miji hiyo, kufuatia ghadhabu zilizochochewa na ukatili wa polisi dhidi ya Mmarekani mwenye asili ya Afrika.

Wanajeshi hao watasaidia polisi wa miji hiyo kulinda amani kuanzia leo.

Soma Habari zote Hapa

Post a Comment

0 Comments