Walinzi wa amani wajeruhiwa DRC


Mpango wa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO, umesema wanajeshi wake wawili wamejeruhiwa katika shambulizi la kulipiza kisasi lililofanywa katika kambi yao, huko katika eneo tete la mashariki ya taifa hilo.

 Katika taarifa hiyo ya MONUSCO iliyotolewa kupitia mtandao wa Twitter, pasipo kutoa ufafanuzi zaidi, imesema washambuliaji waliilenga kambi ya muda ya Umoja wa Mataifa ya Mikange iliyopo jimbo la Kivu ya Kusini. Kwa mujibu wa Radio Okapi, raia watatu pia ni miongoni mwa waliojeruhiwa ingawa jeshi lilisema raia saba

 MONUSCO ni moja kati ya mpango mkubwa kabisa wa amani wa Umoja wa Mataifa duniani, ambao unawajumuisha wanajeshi 16,500 na maafisa wengine raia 4,000. Lakini mpango huo umekuwa katika wakati mgumu kukabiliana na hali ilivyo nchini DRC, kutokana na kuwepo kwa makundi yanayojihami kwa silaha pamoja na kiwango kikubwa cha umasikini na utawala duni.

Post a Comment

0 Comments