Wananchi wa kijiji cha Komarera wamo mbioni kunufaika na fidia ya Barrick



Juzi  mkuu wa wilaya Tarime,Mtemi Msafiri aliwaambia wananchi hao kuwa  eneo lao linahitajika na mgodi wa Barrick na mazungumzo yanaendela ya fidia yakikamilika watatangaziwa malipo.

Msafiri aliwataka wananchi hao kupisha maeneoyanayohitajika kwaajili ya mgodi kufanya shuguli zake na kuwa swala la kutegesha lisiwe na nafasi kwasasa.

Msafiri aliongeza kusema kuwa kwa sasa Mgodi wa Barrick umeingia Ubia na Serikali kwa hali hiyo serikali haihitaji kuona tena Mtu yeyote anaingilia zoezi hilo kwa lengo la kugomesha ama kuvuruga lisifanikiwe tunahitaji zoezi hilo kukamilika kwa wakati .na endapo atabainika Mtu yeyote akigomesha atachukuliwa hatua za kisheria.

"Sisi tumekuja kuwaarifu kuwa Eneo hili la kijiji cha Komarera Mgodi unampango wa kulichukua kwaajili ya shuguli zake Eneo ambalo Mgodi unalihitaji tunawaombeni wananchi na wale ambao walikuwa wanamiliki maeneo hayo kuanzia leo hatuhitaji tena kuona mtu anaendeleza kwa shuguli zake pisheni hadi hapo mazungumzo ya fidia yatakapokamilika"alisema Msafiri.

Mkuu wa wilaya huyo alitumia nafasi hiyo kuwaambia wananchi kuwa watu wale wabaya hawaelewa usemi huo ila wale wazuri wataelewa na kuzingatia kile serikali inachokisema.

Mdhamini mkuuwa Serikali,Evelyne Mugasha alisema kuwa hatagemei tena wananchi kuendelea kutegesha maeneo hayo swala mablo linakwamisha zoezi kutokamilika kwa urahisi na kuwa yeyote ambaye atategesha kuanzia sasa hatafanyiwa tadhimuni na kuwa hatalipwa fidia.

Kiongozi huyo alimaliza kwa kusema kuwa zoezi la udhamini na kuwalipafidia wananchi ni utekelezaji wa Rais John Pombe Magufuli alioutoa wakati kwenye ziara yake wilayani Tarime hapo mwaka 2018.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Komarera,Nyamaganya Marwa alisema kuwa zoezi hilohalijawashirikisha wahusika kwa hali hiyo wananchi wanahitaji mazungumzo yakina ili kuridhia maeneo yaokuchukuliwa kwaajili ya shuguli za mgodi.

Post a Comment

0 Comments