tangazo

Washambuliaji wavamia hospitali moja mjini Kabul

Washambuliaji waliojihami kwa silaha wamevamia na kuishambulia hospitali moja huko magharibi mwa Kabul leo Jumanne na kukabiliana na polisi. 

Watu wanne wameripotiwa kupoteza maisha na wengine watano kujeruhiwa. Hadi sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, ingawa makundi yote ya Taliban na lile linalojiita Dola la Kiislamu IS yamekuwa yakiendesha shughuli zake mjini Kabul na maeneo ya karibu na kuwalenga maafisa wa usalama.

 Moshi mkubwa umeonekana kutokea katika hospitali hiyo iliyoko eneo la Dashti Barchi linalokaliwa zaidi na washia na ambalo limekuwa likilengwa katika siku za nyuma na kundi la IS.

 Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Marwa Amini, amesema polisi tayari wamewasili eneo la tukio ili kukabiliana na washambuliaji. 

Wakati huo kundi la IS limedai kuhusika na mkururo wa mashambulizi ya jana mjini Kabul, ambapo mabomu manne yaliwajeruhi raia wanne.


ADVERTISEMENT

Post a Comment

0 Comments