tangazo

Watanzania waliokwama India kurejeshwa nchini

Ubalozi wa Tanzania nchini India umeeleza kuwa unaendelea kuandaa utaratibu wa kuwarejesha nchini Watanzania waliokwama India.

Katika taarifa yake, ubalozi huo umesema kuwa utahusika katika kuomba vibali vya ndege ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) kutua katika Jiji la Mumbai tarehe 11 Mei 2020 kwa ajili ya safari ya tarehe 12 Mei 2020 ya Mumbai-Dar es Salaam.
Aidha, ubalozi umebainisha kuwa utahusika katika kuwaombea vibali wale wote watakaokuwa wamelipia tiketi ya ndege hiyo ili waweze kutoka sehemu walipo na kufika Mumbai kwa ajili ya safari hiyo.

Ubalozi umewasisitiza Watanzania waliokuwa wamekwama nchini India baada ya kukamilisha matibabu na wanafunzi waliohitimu masomo yao kuchangamkia fursa hiyo adhimu.

Post a Comment

0 Comments