Watu 127 Wathibitishwa kuambukizwa corona leo Kenya


Idadi ya walioambukizwa virusi vya corona nchini Kenya hii leo imefikia 1,745 baada ya watu 127 kuthibitishwa kupata maaambukizi hii leo.

Aidha idadi ya vifo pia nayo imeongezeka na kufikia watu 62 baada ya wengine wanne kuthibitishwa kufa hii leo.

Katibu wa Wizara ya Afya Kenya Dkt. Mercy Mwangangi, amesema kwamba wagonjwa wengine 17 wameruhusiwa kuondoka hospitali katika kipindi cha saa 24 zilizopita huku idadi ya waliopona ikifika 438.

Wakati Bi. Mwangangi anazumgumza, ameonya Wakenya ambao wanatumia njia zisizorasmi kuingia na kutoka katika maeneo ambayo hayaruhusiwi watu kuingia wala kutoka.

"Nataka kuwakumbusha watu kama hao kwamba Nairobi na Mombasa kwa sasa hivi ndio maeneo yenye idadi kubwa ya maambukizi. Kuondoka kwenye kaunti hizo kisiri ni sawa na kusambaza virusi katika kaunti zingine," amesema.

Na kuwafahamisha wenye tabia kama hizo kwamba wanaweza kujiona ni mashujaa lakini huenda ikawa wamesambaza virusi kwa familia na rafiki zao.

"Nawatahadharisha kwamba hatua zitachukuliwa dhidi ya watu kama hao. Nataka kutoa wito kwa watu wa kaunti zingine kuwa makini na kutoa taarifa kwa polisi, iwapo kutakuwa na yeyote ambaye alitoka Nairobi au Mombasa hivi karibuni," Bi Mwangangi amesema.

Aidha amesihi wananchi kwamba ikiwa janga hili ni lidhibitiwe, basi kila mkenya anastahili kuchukua hatua.

Post a Comment

0 Comments