tangazo

Waziri Ummy atoa ripoti ya uchunguzi wa maabara ya kupima Corona

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa ripoti ya Uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na kueleza mambo kadhaa yaliyogunduliwa na Kamati teule ya Uchunguzi

Amebainisha kuwa Kamati imegundua uwepo wa Mapungufu katika mfumo wa kimuundo, kiutendaji na uendeshaji wa kitaaluma katika upimaji wa vipimo, uhakiki wa ubora wa majibu na udhaifu katika uhifadhi wa vipimo vya COVID-19

Amesema mojawapo ya Mashine za kupima sampuli za Covid-19 ilikua na hitilafu bila Uongozi wa Maabara kuchukua hatua za kuifanyia matengenezo kwa wakati

“Upimaji wa Sampuli zote za Covid-19 umehamishiwa katika maabara Mpya iliyokamilika kujengwa katika eneo la Mabibo Dar es Salaam ambayo kwa sasa ndiyo itakuwa maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii.

"Maabara hii mpya ina uwezo wa kupima sampuli 1800 za Ugonjwa wa Covid -19 ndani ya masaa 24 tofauti na ile ya awali iliyokua na uwezo wa kupima sampuli 300 tu.

"Mojawapo ya Mashine za kupima sampuli za Covid-19 ilikua na hitilafu bila Uongozi wa Maabara kuchukua hatua za kuifanyia matengenezo kwa wakati” Amesema Ummy Mwalimu – Waziri wa Afya

Post a Comment

0 Comments