Waziri wa afya amewataka waandishi wa habari kuacha kuandika habari za kuogopesha wananchi kuhusu corona

Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema waandishi wa habari Nchini wanatakiwa kuandika habari sahihi kuhusu corona ili wananchi wapate taaarifa ambazo zitawasaidia kujikinga na ugonjwa huo na sio kuandika habari za kuwaogopesha

Waziri Ummy ameyasema hayo DSM wakati akipokea msaada wa vifaa kinga ,vifaa vya kupimia joto la mwili,vipeperushi, mabango na vifaa vya kutoa elimu kwa waandishi wa habari vilivyotolewa na shirika la UNESCO.

Waandishi pamoja na majukumu yenu ya kazi mnazozifanya hakikisheni mnatoa taarifa sahihi za corona na sio habari za kuwatisha wananchi bali waelimisheni ,nannyi fuateni maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya katika kujikinga na ugonjwa huu hii ikiwa ni pamoja na kusimama umbali wa zaidi ya mita moja kati ya mtu na mtu wakati wakati mnapotekeleza majukumu yenu

Post a Comment

0 Comments