tangazo

Waziri wa mambo ya nje Ujerumani aitaka China iwe wazi kuhusu Corona

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas ameitaka China ishiriki kikamilifu katika uchunguzi wa kubainisha chimbuko la virusi vya corona.

 Waziri Maas ameyaambia magazeti ya shirika la Funke kwamba ulimwengu unataka chimbuko hilo libainishwe kwa uhakika wote.

 Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani ameongeza kusema kuwa majibu sahihi yanapaswa kutolewa na wanasayansi na siyo wanasiasa. Maas amesema China inapaswa kuonyesha wazi jinsi hasa ilivyopambana na virusi vya corona.

Post a Comment

0 Comments