tangazo

Wema Sepetu alamba dili la Ubalozi wa viungo vya mapishi

Dili za ubalozi zinaendelea kumtembelea Msanii wa filamu nchini na Staa wa kipindi cha Mapishi anayefanya vizuri kwa sasa kupitia kipindi chake cha Cook with WemaSepetu mwanadada Wema Sepetu.

Hii ni baada ya leo kutangazwa rasmi kuwa balozi wa sosi ya nyanya (Tomato Sauce) kutoka kampuni ya RedGold.

RedGold ni bidhaa zinazotengenezwa na Darsh Industries Tanzania. Ambapo wana bidhaa nyingine nyingi zikiwemo Tomato Sauce, Chilli Sauce, Jams, Juice na Ketchup.

Aidha, Wema amebainisha kuwa, Kampuni hiyo ya RedGold ndio wadhamini wa kwanza kwenye kipindi chake cha Mapishi kinachoruka kupitia kwenye Application yake iitwayo WemaApp.

Post a Comment

0 Comments