tangazo

Wema Sepetu awatolea uvivu wanaomsakama amekonda

Msanii wa Filamu Bongo, WemaSepetu ambaye kwa sasa anafanya poa kupitia kipindi chake cha mapishi amefunguka kuhusu tuhuma za kuwa amekonda sana kwa sasa.

Akizungumza na U-Heard ya XXL, Clouds FM amesema kwa sasa ameongezeka ila huwa anapenda sana anapokuwa mwembamba kuliko kuwa anapokuwa mnene.

“Uzito sijapima, mara mwisho kupima nafikiri ilikuwa Desemba mwaka jana, nilikuwa na kilo 63 nafikiri sasa nimeongezeka, hadi nikivaa nguo naona nimeanza kubana, sijui napika sana, wewe hujaniona siku nyingi,” amesema.

“Najipenda nikiwa mwembamba,” Wema aliongeza.

Takribani miaka miwili iliyopita mrembo huyo mwenye taji la Miss Tanzania 2006 na C.E.O wa Endless Fame alikiri kufanya aina fulani ya matibabu ili kupunguza unene.

Post a Comment

0 Comments