tangazo

Asilimia 42 ya wanachuo wamewasili na kuanza masomo UDOM

Idadi ya wanafunzi 12,000 sawa na asilimia 42 wamewasili na kuanza masomo katika chuo kikuu cha Dodoma UDOM ikiwa ni siku ya kwanza ya kuanza kwa masomo baada ya likizo ya Zaidi ya miezi miwili kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM Prof. Faustine Bee ameeleza kuwa pamoja na idadi hiyo kuwa chini masomo yameanza hii leo nakutoa wito kwa ambao bado hawajawasili chuoni waharakishe ili kuhitimisha muhula kwa pamoja.

Pia Prof. Bee amewatoa hofu wanafunzi kuwa muhula huu wa masomo utamalizika kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba ili kutoa nafasi kwa wanafunzi kushiriki katika uchaguzi huo kama ambavyo imekuwa ikifanyika miaka yote.

 Habari mpya

Post a Comment

0 Comments