tangazo

Dodoma: Naibu Spika amtembelea Mbowe Hospitali kumjulia hali awatoa hofu Watanzania

NAIBU  Spika, Dkt. Tulia Ackson amewasili katika Hospitali ya DCMC Ntyuka – Dodoma kumjulia hali Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe,  aliyelazwa katika hospitali hiyo akipatiwa matibabu baada ya kuvamiwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana.


“Yupo na mimi nimemuona hapa Hospitali, madaktari wanaendelea kufanya uchunguzi wa vipimo vingine ili kujua ameumia kiasi gani, pengine niwatoe hofu tu Watanzania kwamba anaendelea kupata huduma.
“Kikubwa ambacho kipo ni maumivu ya mguu, yupo na nimemuona wanaendelea na vipimo vingine. Wanaendelea kufanya uchunguzi wa vipimo vingine ili waone ameumia kiasi gani, lakini nikuwaondoa hofu Watanzania kwamba yupo na anaendelea kupata huduma,” amesema Dkt. Tulia.

Post a Comment

0 Comments