tangazo

Freeman Mbowe avamiwa na kushambuliwa

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA Freeman Mbowe amevamiwa na kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake jijini dodoma.

Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene, amethibitisha tukio hilo ambalo lilitokea usiku wa Jumatatu.
Bwana Makene amesema Mbowe kwa sasa anapokea matibabu.
Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika amevieleza baadhi ya vyombo vya habari nchini Tanzania kuwa shambulio hilo lina sura ya kisiasa. Mnyika hata hivyo amesema kuwa taarifa zaidi zitatolewa baadae.
Shambulio dhidi ya Bwana Mbowe linakuja siku moja baada ya mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu kutangaza rasmi nia ya kuwania urais kupitia chama cha Chadema.

Post a Comment

0 Comments