tangazo

Freeman Mbowe: Marekani, EU na Uingereza zaitaka Tanzania kuwakamata waliomshambulia kiongozi wa upinzani.

Muungano wa Ulaya, Marekani na Uingereza zimeshutumu shambulio dhidi ya kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe siku ya Jumanne.
Katika taarifa tofauti zilizowekwa katika tovuti zao, jamii hiyo ya kimataifa imetoa wito kwa serikali ya Tanzania kuanzisha uchunguzi na hatimaye kukamatwa kwa wale wote waliohusika na shambulio la kiongozi huyo wa upinzani.
Freeman Mbowe alivamiwa na kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake jijini Dodoma huku viongozi wa chama chake wakidai kwamba shambulio hilo lilishinikizwa kisiasa.
Marekani imetoa wito kwa serikali ya Tanzania kuanzisha uchunguzi na hatimaye kukamatwa kwa wale wote waliohusika na shambulio la kiongozi wa upinzani nchini humo Freeman Mbowe.
Freeman Mbowe alivamiwa na kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake jijini Dodoma huku viongozi wa chama chake wakidai kwamba shambulio hilo lilishinikizwa kisiasa.
Kulingana na taarifa iliochapishwa katika tovuti ya ubalozi wake nchini humo, imesema kwamba unaliona tukio hilo kama la kikatili na lisilo na sababu.
''Ubalozi wa Marekani umeshtushwa na kuhuzunishwa na tukio la kikatili la kushambuliwa kwa mbunge na mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe tarehe 9 Juni, tunatoa pole kwa mbunge huyo na familia yake'',ilisema taarifa hiyo.

Ikumbukwe hakuna nchi tulivu na yenye amani duniani kama Tanzania, siasa zake nizaupendo Uhuru na kila raia ana haki sawa na mwenzake.

Jambo hili halina uhusiano wowote kisiasa na serikali. Viongoze wote wa serikali ya Tanzania wameonesha kusikitishwa na hali hii iliyojitokeza. Waziri mkuu na viongozi wengine tayari wamekwisha kwenda kumjulia hali hospitali alipolazwa kwa matibabu kiongozi huyo.

Post a Comment

0 Comments