George Floyd: Trump asema kambi za kijeshi zenye majina ya majenerali waliotukuza utumwa ni turathi ya Marekani

Rais wa Marekani Donld Trump anasema kwamba hatofikiria kubadilisha majina ya kambi za kijeshi zilizotajwa baada ya majenerali walioongoza jeshi la Marekani.
Alituma ujumbe wa twitter akisema kwamba kambi hizo ni miongoni mwa turathi kuu za Marekani.
Matamshi hayo ya bwana Trump yanajiri kufuatia ripoti kwamba maafisa wakuu wa jeshi walikuwa tayari kuruhusu mabadiliko kufuatia maandamano yaliosababishwa na kifo cha George Floyd.
Kwa wengi, alama za mataifa ya kusini yaliokuwa yakiwahifadhi watumwa ambayo baadaye yalijiondoa katika biashara hiyo na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe Amerika - zilikuwa na kumbukumbu za kibaguzi.

Je Trump alisemaje?

Bwana Trump alituma ujumbe wa twitter siku ya Jumatano kwamba kambi za kijeshi zilizopatiwa majina ya majenerali waliohusika katika biashara ya utumwa zimekuwa miongoni mwa turathi muhimu za historia ya Marekani, historia ya kushinda, ushindi na Uhuru.
Aliongezea: "Marekani iliwapatia mafunzo na kuwapeleka mashujaa wetu katika maeneo hayo ,na kufanikiwa kushinda vita viwili vya duniani. Hivyobasi utawala wangu hautafikiria kubadilisha majina ya kambi hizi na hata vifaa vya kijeshi.Historia yetu kama taifa lenye uwezo mkubwa duniani haitaingiliwa, Heshimuni jeshi letu.
Afisa anayesimamia masuala ya habari katika Ikulu ya Whitehouse Kayleigh McEnany alisema katika taarifa kwa vyombo vya habari baadaye kwamba uwezekano wa kubadilisha majina ya kambi hizo za kijeshi , haupo kwa rais Trump.
Alisema kwamba hatotia saini sheria yoyote ambayo itapitishwa na bunge la Congress inayohitaji majina hayo kubadilishwa.

Je ni nini kilimchochochea Trump kutuma ujumbe wa Twitter?

Siku ya Jumatatu maafisa wa Pentagon walisema kwamba waziri wa ulinzi Mark Esper na katibu wa jeshi Ryan McCarthy walikuwa tayari kuingia katika majadiliano yasiopendelea upande wowote kuhusu mada ya kubadilisha majina ya majenerali waliohusika katika kutukuza utumwa.



Kifo cha Floyd: Wamarekani weusi wasema 'hawako salama'

Mapema wiki hii, jeshi la wanamaji wa Marekani lilitoa agizo kwa makamanda kutambua na kuondoa bendera za vita hivyo katika maeneo ya kazi, maeneo ya maarufu na yale ya umma.
Katika taarifa siku ya Jumanne , jenerali mstaafu David Patraeus aliandika kuhusu wakati wake akiwa katika kambi ya Fort Brag: Kejeli ya kujifunza katika majina yaliotajwa baada ya wale waliochukua silaha dhidi ya jeshi la Marekani na haki ya kuwafanya wengine kuwa watumwa haitakubalika kwa mtu yeyote anayelifikiria suala hili."
Kambi 10 zilizotajwa majina ya majenerali waliohusika katika utumwa ni pamoja na Fort Bragg iliopo North Carolina, Fort Hood mjini Texas na Fort Benning mjini Georgia.
Zote zipo katika majimbo ya kusini ambayo yalimsaidia bwana Trump kupata ushindi 2016 na anayategemea kumpatia ushindi tena katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Presentational grey line

Je ni fursa iliopotea?

Saa moja kabla ya rais kufanya kikao na wafuasi wake weusi , alikuwa akituma ujumbe katika twitter kuhusu pingamizi yake ya kuyabadilisha majina ya kambi hizo.
Huenda inashangaza kwa Marekani kuwa na kambi za kijeshi zilizotajwa majina ya maafisa walioongoza jeshi dhidi ya majeshi ya Marekani, lakini hayo ni mapungufu ambayo yamesalia kuwepo zaidi ya miaka 150 baada ya kukamilika kwa vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe.
Wengine bado wanawachukulia majenerali hao kuwa mashujaa kwa fursa iliopotea.
lakini hilo halijazuia serikali za mitaa na zile za kijimbo kuondoa sanamu zao. Rais huyo hatahivyo amekataa kubadilisha msimamo.
Ameunga mkono kile anachokiita sanamu 'nzuri' na yuko tayari kuanza vita ili kuhifadhi majina yao katika vifaa vya serikali.
Hata wakati ambapo raia wa Marekani wanafikiria kuhusu ubaguzi uliopo, rais ameamua kwamba hatokubali kurudi nyuma.

Presentational grey line

Je ni nani mwengine anataka kuondolewa kwa alama hizo?

Kifo cha George Floyd , baada ya afisa wa polisi mzungu kumwekea goti katika shingo yake mjini Minneapolis , Minnesota, kiligusa donda la ubaguzi wa miaka mingi nchini Marekani.
Siku ya Jumatano Spika wa bunge la uwakilishi nchini Marekani Nancy Pelosi alitoa wito wa sanamu zilizotukuza utumwa katika mji mkuu wa Washinton DC kuondolewa.
"Sanamu za watu waliounga mkono ukatili ili kufanikisha ubaguzi uliopo ni suala linaloch''ukiza kwa kweli, alisema mwanachama huyo wa Democrat kutoka jimbo la California.
''Sanamu hizo zinaleta chuki na sio turathi, zinapaswa kuondolewa''.

Post a Comment

0 Comments