tangazo

Jux alipa zaidi ya milioni 26

MKALI wa RnB Bongo, Juma Musa ‘Jux’ amesema kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania wanaolipa kodi kubwa serikalini kupitia biashara yake ya nguo.  Jux ameliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, bidhaa zake za nguo za African Boy zimempa mafanikio makubwa.

“Mimi ni mmoja kati ya wafanyabishara na wasanii ambao wanalipa kodi kubwa serikalini. “Kontena langu moja moja nalipa kati ya shilingi milioni 26 hadi 27 na kwa mwaka naingiza kontena mbili hadi tatu,” amesema Jux.

Jux amesema kwa sasa ana duka la jumla Kariakoo jijini Dar na Uganda huku akiwa na malengo ya kutanua biashara yake Afrika na duniani.

Staa huyo wa wimbo wa Sugua amesema kwa sasa biashara hiyo anaimiliki kwa asilimia mia moja huku akisema biashara ikitanuka na kuanza kuzaa matunda zaidi ataanza kuuza hisa.

Post a Comment

0 Comments