Kaburi la umati lagunduliwa kusini mwa Libya

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya imetangaza kuwa imegundua kaburi la umati katika eneo lililokombolewa kutoka kwa wapiganaji wanaoongozwa na jenerali muasi, Khalifa Haftar.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Libya imesema kuwa kaburi hilo la umati limegunduliwa huko kusini mwa Tripoli katika eneo la Saadiyya lililokombolewa kutoka kwa wapiganaji wa Haftar

Kaburi hilo lina miili ya familia moja inayojumuisha baba, mama na watoto wao wawili.

Tangu Aprili mwaka jana wapiganaji wa jenerali muasi, Khalifa Haftari walianzisha mashambulizi makubwa katika jitihada za kuuteka mji wa Tripoli, suala ambalo limelaaniwa na jamii ya kimataifa. Zaidi ya watu 1,500 wameuawa katika mashambulizi hayo na wengine wasiopungua 6,000 wamejeruhiwa. Watu laki moja na nusu pia wamelazimika kuwa wakimbizi.

Mwezi Aprili mwaka jana wakati juhudi za kuutatua kisiasa mgogoro wa Libya zilipokuwa zimekaribia kuzaa matunda, jenerali huyo muasi alianzisha mashambulizi ya pande zote dhidi ya mji mkuu Tripoli akisaidiwa na Saudi Arabia, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na baadhi ya nchi za Magharibi. Hata hivyo ndoto yake hiyo imeshindwa kutimia kutokana na muqawama wa Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa iliyoundwa na Umoja wa Mataifa.

Historia na Mabaki ya Kale Tanzania


Post a Comment

0 Comments