tangazo

Kauli ya CHADEMA baada ya Mbowe kuitwa mlevi

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tumaini Makene amesema kuwa chama hicho hakiwezi kujibishana na wale wote waliotoa kauli za kwamba, Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe alilewa na kudondoka na si kushambuliwa kama chama kilivyosema.

Hayo ameyabainisha leo Juni 10, 2020, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio na kuongeza kuwa, wao ni hadhi ya juu hivyo wakisema wabishane nao watajishusha na kufanana nao, sababu kauli walizozitoa jana ndiyo zile zile walizozitoa Lissu aposhambuliwa kwa risasi.

"Ni vitu ambavyo mimi sikutaka kuvizungumza kwa sababu, ukizungumzia unajishusha kwenye level yao ya kufikiria, watu wengi wamewadharau na kuwapuuza, watu hao hao waliyoyazungumza maneno tunayoyasikia, ndiyo wale wale waliosema Lissu alijipiga risasi" amesema Makene.

Aidha Makene akizungumzia suala la kiongozi wa chama hicho kukosa walinzi, hali iliyopelekea kushambuliwa na watu wasiojulikana amesema kuwa, "Baada ya tukio la Lissu ilitungwa sheria ya vyama vya siasa, ambayo imepiga marufuku viongozi wa vyama vya siasa kujilinda, hilo swali inabidi muwaulize watawala wakati wanatunga sheria hii walijua litakalokuja kutokea baadaye?".

Post a Comment

0 Comments