tangazo

Kiongozi wa upinzani Malawi ashinda uchaguzi


Kiongozi wa upinzani nchini Malawi Lazarus Chakwera ameshinda uchaguzi  wa  wiki  hii  wa  rais ulioamriwa  kufanyika  tena kwa asilimia 58.57 ya kura, tume ya uchaguzi ya nchi hiyo imesema.

Ilikuwa  ni  mabadiliko  makubwa ya majaaliwa  kwa  kiongozi aliyeko madarakani, Peter Mutharika, ambaye  ushindi  wake  katika uchaguzi  wa  mwezi  Mei  2019 ulibatilishwa na mahakama  ya katiba, yakihusishwa  na  udanganyifu  mkubwa.
Kiasi ya  wapiga  kura  milioni 6.8  katika  taifa  hilo  dogo  la  kusini mwa  Afrika walijitokeza  katika  vituo vya  kupigia  kura  siku  ya Junanne. Na  jana  Jumamosi , tume  ya  mwenyekiti  wa  tume  ya uchaguzi  Chifundo Kachale aliwaambia  waandishi  habari; "Tume imemtangaza Lazarus Chakwera , kwa  kupata  asilimia 58.57 ya kura, kuwa  amechaguliwa  kuwa  rais wa  Malawi.
Mutharika  alikuwa  wa  pili  kwa  kupata  kura  1,751,377, wakati mgombea  ambaye  hajulikani  sana  Peter Dominico Kuwani amepata  kuwa 32,456.
Watu waliojitokeza  kupiga  kura  ni  asilimia 64.81.

Bofya Soma Habari Zingenezo Hapa

Post a Comment

0 Comments