Kwa nini picha hii huzifanya simu kujizima?

Kwanini picha hii huzifanya simu kujizima?
Picha ya ardhi yenye mandhari ya kuvutia , iliyo na ziwa huku jua likitua nyuma ya milima inaonekana nzuri kwa mtu kutumia katika simu yake.
Lakini Baadhi ya watumiaji wa simu zinazotumia mfumo wa Android wameshangazwa kugundua kwamba simu zao zinajizima wanapotumia picha hiyo.
Baadhi ya simu zilizoathirika na picha hiyo kama vile Samsung na Google Pixel ni miongoni mwa zilizotuma ripoti ya malalamishi.
Makosa ya mfumo wa Andoid hufanya kioo cha simu kujizima na kujiwasha mara kwa mara baada ya picha hiyo kutumika kama picha ya msingi ya kupamba simu{ Wallpaper}.
Mara nyingine simu hulazimika kurudisha programu hiyo ya Android kupitia huduma ya mpangilio wa programu inapopotea. BBC haipendekezi uitumie.
Samsung tayari imeripoti kwamba itatoa majibu yake Juni 11 ili kurekebisha makosa hayo.
BBC ilijaribu kupata tamko kutoka Google , lakini haikupata jibu la haraka.
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamearifu kuhusu tatizo hilo.
''Iwapo mtu anakutumia , tafadhali ipuuzilie mbali'', onyo moja lililosambazwa sana katika Twitter lilisema.
Msitumie picha hii kama picha ya kupamba simu zenu[ Wallpaper} , hususan katika simu za Samsung.
Itasababisha simu yako kupoteza data!
Usijaribu!
Mtu anapokutumia picha hii tafadhali ipuuze.
Wanahabari wa masuala ya teknolojia Bogdan Petrovan amesema kwamba kirusi hicho hakikuathiri simu yake aina ya Huawei 20 Pro, lakini kilizuia simu ya Google Pixel 2 kutofanya kazi.
"Baada ya kuweka picha yenye utata kama wallpaper, simu hiyo ilijifunga''.
''Nilijaribu kuiwasha upya, lakini kioo kilijizima na kujiwasha mara kwa mara, hatua inayofanya kuwa vigumu kuingia katika programu ya usalama wa simu'', alisema.
''Kuiwasha upya simu hiyo kupitia programu salama {kwa kubonyeza kitufe cha sauti ili kuianzisha} hakutatua tatizo hilo'', aliongezea.

Je ni nini kinachoendelea?

Kirusi hicho kinaonekana kuathiri baadhi ya simu lakini sio simu zote zinazotumia mfumo wa Google wa operesheni za simu , kwa jina Android 10.
Ken Munro na Dave Lodge, wanaoshirikiana na kampuni ya usalama wa teknolojia Pen Test, walitoa uchangaunzi wao kwa BBC.
"Kwasasabu picha za kidijitali zimeimarika ubora , simu lazima ziweze kutazama kile kilichopo katika nafasi ya rangi hiyo ili kubaini jinsi itakavyoionyesha vizuri'', alisema.
''Hivi ndivyo jinsi simu inagundua kutoa kuvuli kilicho sawa cha rangi ya kijani, kwa mfano'' waliendelea.
Android.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBaadhi ya simu zilizoathirika na picha hiyo kama vile Sansung na Google Pixel
Kuna njia tofauti kubaini nafasi ya rangi. Baadhi ya nafasi nyengine zina matumizi maalum katika muundo wa picha hivyobasi wakati mwengine unaweza kutazama picha ambazo haziko katika mfumo wa kawaida wa RGB.
''Pia inawezekana kubuni kwa makusudi picha ambazo zina habari nyingi kuhusu rangi ambazo baadhi ya simu zinaweza kushughulikia, aliendelea.
Kile kilichofanyika hapa ni kwamba baadhi ya simu huliangazia suala hili kimakosa.
''Simu hufeli kwasababu haijui kushughulikia sawasawa na watengenezaji wa programu huenda pengine hawakufikiria kwamba hilo linaweza kutokea'', walitamatisha.

Post a Comment

0 Comments