Maelfu waandamana kupinga ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi

Katika kile kinachoelezwa kuwa ni maandamano makubwa zaidi kushuhudiwa, dhidi ya ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi, maelfu ya waandamanaji wameshiriki Marekani na maeneo mengine ya ulimwengu.
Makamo wa rais wa zamani wa Marekani Joe Biden ametumia mwanya huo kujipigia chapuo kisiasa kwa kutetea mabadiliko ya muundo wa jeshi la polisi kwa kile alichokiita hatua muafaka ya muda mrefu, sera kamili ya kubadili ubaguzi wa kimfumo. Endapo atachaguliwa katika uchaguzi wa Novemba.
Kupitia gazeti la kila siku la mjini Los Angeles, Los Angeles Times, amesema kama atachaguliwa ataunda kamisheni ya polisi ya taifa itakayoshughulikia masuala hayo ndani ya siku 100 akiwa ofisini.

Maafisa wawili wa polisi wa Buffalo wameshitakiwa


Wakati hayo yanaelezwa maafisa wawili wa polisi  katika jiji la Buffalo, katika jimbo la New York wameshitakiwa kwa kufanya shambulizi, baada ya kuonekana katika video wakimsukuma mwandamanaji mzee wa umri wa miaka 75, wakati wa maandamano ya kupinga mauwaji ya Katika video hiyo, mzee huyo alionekana akianguka chini, kichwa chake kujigonga katika lami, akapoteza fahamu na kuanza kuvuja damu.
Katika mji wa kaskazini/magharibi wa Marekani wa Seattle, kumeshuhudiwa maandamano ya siku ya tisa mfululizo, kufuatia kifo cha Floyd. Kundi kubwa la wafanyakazi wa sekta ya afya, na wengi wao wakiwa wamevaa mavazi ya maabara wameshiriki maandamano hayo. Mwanadamaji mmoja alibeba bango lilioandikwa "Wauguzi wanapiga magoti nawe, sio kukupigia wewe." Na mwengine "Ukatili wa polisi na ubaguzi ni dharura ya afya ya umma."

Post a Comment

0 Comments