tangazo

Marekani yaiomba China kuwaachia Raia wawili wa Canada

Marekani imetoa wito wa kuachiliwa huru kwa raia 2 wa Canada wanaoshikiliwa nchini #China kwa tuhuma za kufanya ujasusi nchini humo

China inawashikilia Michael Kovrig, Mwanadiplomasia wa zamani na Mfanyabiashara Michael Spavor. #Marekani imelaumu kuwa hakuna sababu za msingi za kuwashikilia raia hao ambapo Mahakama kuu ya #China imeanza kusikiliza kesi ya 2 hao

Hatua hiyo ni kama kisasi kwa kuwa #Canada inamshikilia Mkurugenzi wa Kampuni ya Huawei, Meng Wanzhou kwa madai ya kuwa kampuni yao ilikiuka masharti ya vikwazo dhidi ya Iran

Kesi hizi mbili zimeendelea kuhatarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Mataifa hayo mawili na hata kuyumbisha shughuli za kibiashara kati ya mataifa hayo

Post a Comment

0 Comments