tangazo

Mbosso, Diamond washinda tuzo za Hipipo Uganda


Tuzo kubwa za muziki nchini Uganda , Hipipo Music Awards (Hall of Fame) , zimefanyika siku ya Jana huko Kampala na Kushuhudia wasanii tokea Lebo ya WCB , Diamond Platnumz pamoja na Mbosso wakiiwakilisha vyema Tanzania kwa Kuondoka na jumla ya tuzo tatu (3)

Katika tuzo hizo ambazo mwaka huu zimefanyika bila sherehe kutokana na Janga la Corona , Diamondplatnumz ameondoka na tuzo mbili ambazo ni Wimbo bora wa Afrika Mashariki (THE ONE) na Msanii Bora wa Tanzania. Huku Mbosso_Mshedede akishinda tuzo ya Africa Fans Favorite Fresh Talent (Msanii mpya , Kipenzi cha Mashabiki Barani Afrika)

Habari za Mastaa

Post a Comment

0 Comments