Mtanzania atambulika kuwa bilionea baada ya kupata mawe makubwa ya Tanzanite



WIZARA YA MADINI TANZANIA TWITTER

Mtanzania Saniniu Lazier ambaye ni mchimbaji madini mdogo amepata madini ya Tanzanite ambayo ya thamani ya bilioni 7.8.
Madini Hayo ambayo moja lina kilo 9.2 lina thamani ya bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani ya shilingi bilioni 3.3.
Aidha baada ya kupata madini hayo bwana Laizer aliyafikisha katika kituo cha utambuzi. Na hii leo serikali ya Tanzania imeyanunua madini hayo kwa thamani ya bilioni saba na milioni mia saba za kitanznaia.
Madini hayo yamekabidhiwa kwa serikali na bwana Lazier ambaye ni mkazi wa Simanjiro amepatiwa fedha zake huko Mkoani Arusha kaskazini kwa Tanzania.


Mchimbaji mdogo wa madini Saniniu Laizer ametangazwa kuwa bilioneaHaki miliki ya pichaWIZARA YA MADINI TWITTER

Kupitia mtandao wa Twitter wizara ya madini ya Tanzania imemtambua mtanzania huyo kama bilionea.
Kwa mujibu wa wizara ya madini nchini humo maadini ya uzito huo hayajawahi kupatikana katika machimbo ya Tanzanite
Tanzanite ni madini yanayopatikana na kuchimbwa nchini Tanzania pekee.
Mauzo ya madini hayo kwa mwaka 2019 duniani yalikua zaidi ya dola milioni 50 za kimarekani.

Haya yote yametokana na uongozi wa awamu ya tano ya Rais John Magufuri kuanzisha masoko ya madini ya ndani na ujenzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Milelani.

Post a Comment

0 Comments