tangazo

Ndege ya kwanza ya abiria yatua KIA,Yapokelewa na Waziri Kigwangala na pia yapigiwa salute

Ndege ya shirika la Ndege la Ethiopian Airline imetua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ikitokea Dubai ikiwa imepita takribani miezi mitatu tangu zilipositishwa safari za ndege kuoka nje ya nchi kutokana na tahadhari ya maambukizi mapya ya virusi vya Corona.
Majira ya saa 11:00 za jioni katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Lilimanjaro (KIA) , Clouds 360 imeshuhudia ndege hiyo iliyobeba watalii ikiwasili katika uwanja huo na kulakiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangala aliyekuwa ameongozana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na watoto, Dkt ,Godwin Molel .

Post a Comment

0 Comments