Nukuu (Quotes) 30 za Mafanikio zitakazokuhamasisha

Kila mtu ana maana yake ya mafanikio. Ni wazi kuwa mafanikio ni kuweza kukabiliana na changamoto au kushindwa bila kukata tamaa au kuacha.

Mara nyingi huwa napenda kusoma nukuu (Quotes) mbalimbali kwani huwa zinanipa hamasa kubwa ya kuzidi kufanyia kazi ndoto zangu.

Naamini hata wewe unaweza kuhamasika na kupata ari zaidi kwa kusoma nukuu hizi 30 za mafanikio.

1. “Ni bora kushindwa kwenye kitu halisi kuliko kufanikiwa kwenye kitu cha kuiga.”
-Herman Melville

2. “Njia ya kufanikiwa na barabara ya kushindwa ni sawa kabisa.”
  -Colin R. Davis

3. “Mafanikio huja kwa wale ambao wanafanya bidii kubwa kuyatafuta.”
-Henry David Thoreau

4. “Usijaribu kuwa mtu wa mafanikio. Bali jaribu kuwa mtu wa thamani.”
-Albert Einstein

5. “Acha kukimbilia pesa bali anza kukimbilia shauku yako.”
-Tony Hsieh

6. “Mafanikio ni kupita kutoka aina moja ya kushindwa hadi nyingine bila kukata tamaa.”
-Winston Churchill

7. “Fanya kitu kimoja kila siku kinachokutisha.”
-Hajulikani

8. “Ukitazama kwa karibu, mafanikio ya usiku mmoja huchukua muda mrefu.”
-Steve Jobs

9. “Hakuna siri ya mafanikio, ni matokeo ya maandalizi, kufanya kazi kwa bidii, na kujifunza kutokana na kushindwa.”
-Colin Powell

10. “Inaonekana mafanikio yameungwa na matendo. Watu waliofanikiwa wanaendelea mbele. Wanafanya makosa lakini hawaachi.”
-Conrad Hilton

11. “Kama unataka kufanya kitu, utatafuta njia. Kama hutafanya hivyo, utatafuta kisingizio.”
-Jim Rohn

12. “Siwezi kukupa kanuni ya mafanikio, lakini ninaweza kukupa kanuni ya kushindwa – nayo ni: Jaribu kumridhisha kila mtu.”
-Herbert Bayard Swope

13. “Mafanikio siyo ufunguo wa furaha. Furaha ni ufunguo wa mafanikio. Kama unapenda unachokifanya, utafanikiwa.”
-Albert Schweitzer

14. “Mafanikio siyo vitu ulivyokamilisha kwenye maisha yako, bali ni nini ulichowahamasisha wengine kufanya.”
-Hajulikani

15. “Baadhi ya watu wengine wanaota mafanikio wakati wengine wanaamka na kufanya kazi.”
-Hajulikani

16. “Mtu mwenye mafanikio ni yule anayeweza kujenga msingi imara kwa kutumia matofali yaliyotupwa na wengine.”
-David Brinkley

17. “Ili kufanikiwa ni lazima tuamini kuwa tunaweza.”
-Nikos Kazantzakis

18. “Kushindwa kwingi kwenye maisha ni watu wanaoshindwa kufahamu jinsi walivyo karibu na mafanikio wanapokata tamaa.”
-Thomas Edison

19. “Mafanikio ni kupata unachotaka, furaha ni kutaka unachopata.”
-Dale Carnegie

20. “Eneo baya la mafanikio ni kujaribu kutafuta mtu ambaye ana furaha kwa ajili yako.”
-Bette Midler

21. “Usipoteze muda kupiga ukuta, ukitumaini kuubadili kuwa mlango.”
-Coco Chanel

22. “Nimefanikiwa leo kwa sababu nilikuwa na rafiki aliyeniamini na sina moyo wa kumwangusha.”
-Abraham Lincoln

23. “Yote unayohitaji kwenye maisha yako ni ujinga na ujasiri; kisha mafanikio ni hakika.”
-Mark Twain

24. “Ili kufanikiwa, shauku yako ya mafanikio ni lazima iwe kubwa kuliko hofu yako ya kushindwa.”
-Bill Cosby

25. “Changamoto kubwa baada ya kufanikiwa ni kunyamaza kuhusu mafanikio hayo.”
-Criss Jami

26. “Mafanikio hayahusishi kutokufanya kosa bali kutokurudia kosa hilo mara ya pili.”
-George Bernard Shaw

27. “Mafanikio ni pale ambapo maandalizi na fikra vinakutana.”
-Bobby Unser

28. “Kila mara kujiamini na bidii kutakupa mafanikio.”
-Virat Kohli

29. “Mafanikio siyo mwalimu mzuri, kushindwa hukufanya kuwa mnyenyekevu.”
-Shah Rukh Khan

30. “Kabla ya kitu kingine chochote, maandalizi ni ufunguo wa kufanikiwa.”
-Alexander Graham Bell

Naamini umehamasika na kupata shauku zaidi ya kufanyia kazi malengo na ndoto zako ili ufanikiwe. Kila kitu kinaanza kwenye fikra zetu.

Naamini umebaini wazi kuwa maana ya mafanikio ni pana; pia mafanikio siyo kutokukabiliana na changamoto bali ni kuzikabili.

Post a Comment

0 Comments