Rais wa Zanzibar “kutawaliwa sio kuzuri, mtawala anafanya anavyotaka”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein katika kikao cha ndani kilichofanyika Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Makamu Mwenyekiti CCM Bara Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally Kakurwa ambapo viongozi hao wamezungumzia masuala ya CCM.
Baada ya kikao hicho, Rais Shein amekwenda kuweka udongo katika jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Ikulu na kukagua maendeleo ya kazi ya ujenzi wa ofisi hizo inayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia shirika lake la Suma JKT.
Rais Shein amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumpa fursa ya kwenda kuweka udongo ikiwa ni kumbukumbu ya ujenzi wa ofisi hizo na amebainisha kuwa kujengwa kwa ofisi hiyo ni heshima kwa Taifa na tafsiri sahihi ya kujitawala.
Rais Shein amewasalimu vijana wa JKT wanaofanya kazi za ujenzi wa ofisi hizo, amewapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya na amewataka kujivunia fursa hiyo adhimu ya kujenga ofisi ya Ikulu za nchi yao, badala ya kazi hiyo kufanywa na kampuni za nje ya nchi kama ambavyo hufanyika katika maeneo mengi.

MSIBA WAGEUKA SHEREHE MOSHI NI WA BINADAMU MZEE KULIKO WOTE DUNIANI

Post a Comment

0 Comments