RPC Muroto atoa onyo kali kuhusu tukio la Mbowe

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto, amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA ambapo ameonya watu kutotumia tukio hilo kisiasa.

Muroto amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma, kutoa taarifa juu ya shambulio ambalo amefanyiwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freema Mbowe.

''Onyo kali kwa wanasiasa na mtu yeyote atakayetumia tukio hili kwa namna yoyote ile ikiwemo kujiongezea umaarufu au kuingilia uchunguzi wa polisi, tutamshughulikia kweli'', amesema.

Aidha amethibitisha kweli kushambuliwa kwa Freeman Mbowe na amesema wanaendelea na uchunguzi ikiwemo kuwahoji majirani na watu wengine huku akisisitiza kuwa hataachwa mtu yeyote ambaye anahusika.

Post a Comment

0 Comments