Serikali yaandaa mfumo wa Kielektroniki Uhakiki madeni hewa

Serikali inaandaa mfumo wa kielektroniki, utakaotumika katika kukusanya na kulipa madeni yote ya watumishi wa umma, ili kuondokana na tatizo la udanganyifu kunakosababisha kuwepo kwa madeni hewa.
Mpango huo wa serikali umetangazwa jijini Dodoma na Rais Dkt. John Magufuli, wakati alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Nchini (CWT), unaoambatana na uchaguzi mkuu wa viongozi wa chama hicho, na kusisitiza serikali inaendelea kulipa madeni ya watumishi wake wakiwemo walimu, lakini ni baada ya kuyahikiki madeni hayo.

Pamoja na mambo mengine, Rais akachukua wasaa huo kuwahimiza watanzania kwa mara nyingine tena, kuacha kupokea misaada ya barakoa wasizozijua zinatoka wapi, huku akiwakumbusha viongozi wa ngazi mbalimbali wajibu wao wa kuwalinda wananchi.

Post a Comment

0 Comments