Tetesi za soka Jumatatu 01.06.2020: Sane, Havertz, Telles, Osimhen, Werner, Camavinga


Bayern Munich wanataka kumsajili winga wa Manchester City Leroy Sane

Bayern Munich wanataka kumsajili winga wa Manchester City, raia wa Ujerumani Leroy Sane , 24,na Kai Havertz, 20, kutoka Bayer Leverkusen kama sehemu ya ''enzi mpya'' katika klabu, amesema Makamu Mwenyekiti. (Bayern1 via Evening Standard)
Chelsea inaiongoza Paris-St Germain katika kinyang'anyiro cha kumnasa beki wa kushoto wa Porto na raia wa Brazil Alex Telles, 27. (Tuttosport via Express)
Lille wamepata ofa nyingi kwa ajili ya mshambuliaji wao Osimhen. Tottenham, Liverpool na Arsenal ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka Mnaijeria huyo,21, (Mail)
Mshambuliaji wa RB Leipzig na mchezaji anayetolewa macho na Liverpool Tino Werner ameweka wazi uamuzi kuhusu mustakabali wake katika mazungumzo kuhusu uhamisho wake, ameeleza Mkurugenzi wa michezo wa Inter Milan Piero Ausilio. Ausilio amesema Mjerumani huyo, 24, ''hatakuja kwetu''. (Daily Star)
Arsenal wanapendelea kumpata mshambuliaji wa Napoli Arkadiusz Milik,26, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Juventus (La Repubblica via Daily Star)
Manchester United wanaamini wakala Mino Raiola ni mtu pekee anayetaka Paul Pogba kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu. Kiungo wa Ufaransa Pogba, 27, amehusishwa na taarifa za kuhamia Real Madrid na Juventus. (Times-subscription)

Tino WernerHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTino Werner

Rennes wameamua kumuuza mchezaji aliyekuwa akitolewa macho na Liverpool na Real Madrid Eduardo Camavinga msimu huu. Kiungo huyo wa kati pia anahusishwa na taarifa za kuelekea Manchester United. (RTL via Evening Standard)
Kiungo wa kati wa Liverpool Harvey Elliot amekacha nafasi ya kujiunga na Real Madrid. Muingereza huyo, 17, alikuwa amealikwa kukutana na Sergio Ramos katika jaribio la kumshawishi kujiunga. (The Athletic)
Barcelona itatafuta pauni milioni 9 kama ada ya mkopo kutoka kwa klabu yoyote ya ligi ya primia kwa ajili ya kiungo wa kati na raia wa Brazil Philippe Coutinho.(Mundo Deportivo via Mirror)
Kiungo wa Atletico Madrid na mchezaji anayefikiriwa pia na Manchester United Saul Niguez amesema atatangaza ''klabu mpya'' ndani ya siku tatu zijazo. Raia huyo wa Uhispania, 25, mkataba wake na timu ukitaka kuweka mezani kitita cha pauni milioni 130 ili kumnyakua .(Manchester Evening News)

Saul NiguezHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSaul Niguez

Everton wanatarajiwa kumuita tena mlinda mlango Jonas Lossl, 31, baada ya mkataba wake wa kucheza kwa mkopo kumalizika katika klabu ya Huddersfield Town. (Yorkshire Evening Post)
Celtic wanafikiria kumsajili mlinda mlango wa Manchester City raia wa Chile Claudio Bravo, 37. (Times-in Spanish)
Kocha wa Chelsea Frank Lampard amesema ''atafanya maboresho '' katika kikosi chake katika dirisha kubwa la usajili (Mail)
Inter Milan wamesema kuwa wanataka kuendelea kumshikilia mshambuliaji wa Manchester United Alexis sanchez kwa mkopo baada ya tarehe 30 mwezi Juni. Mchezaji huyo anaichezea klabu hiyo ya ligi ya Serie A mpaka mwishoni mwa msimu. (Sky Sports Italia).


Post a Comment

0 Comments