tangazo

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 11.06.2020: Sancho, Zaha, Bertrand, Fraser, Cazorla,


Borussia Dortmund kumuuza Jadon Sancho kwa pauni milioni 115

Borussia Dortmund itahitaji kulipwa pauni milioni 115 ili kumuuza mchezaji wa England mwenye umri wa miaka 20 Jadon Sancho. (Telegraph)
Winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 27 anavutia hamu kutoka kwa klabu ya Paris St-Germain. (90 Min)
Southampton inapanga kuanza mazungumzo ya kandarasi mpya na beki wa kushoto Ryan Bertrand, 30, huku klabu ya Leicester ikivutiwa na mchezaji huyo.(Daily Mail)

Wilfried ZahaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionParis St-Germain inamnyatia Winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha

Kipa wa Bournemouth na Poland Artur Boruc, 40, kiungo wa kati wa England Andrew Surman, 33, beki wa England Simon Francis, 35, na Charlie Daniels, 33, wanatarajiwa kuandikisha mikataba mifupi na klabu hiyo . (Bournemouth Echo)
Uwezekano wa Chris Hughton kurudi kuifunza Birmigham ni mdogo. (Birmingham Mail)
Kiungo wa kati wa uskochi Ryan Fraser, 26, anatarajiwa kukataa ofa ya muda mfupi katka klabu ya Bournemouth, ikimaanisha anaweza kuondoka kama mchezaji huru mwisho wa msimu huu. (Sun)

Ryan FraserHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRyan Fraser(Kulia) amefungia Bournemouth bao moja tu msimu huu

Manchester United itakabiliana na West Brom katika mechi mbili za kirafiki katika uwanja wa Old Trafford siku ya Ijumaa, huku ikijiandaa kurudi kwa ligi ya Premia siku ya Ijumaa. (Telegraph)
Kiungo wa kati wa klabu ya Uhispania na Villarreal Santi Cazorla, 35, anasema kwamba amefanya uamuzi wake kuhusu hatma yake - lakini hatofichua chochote. Kandarasi ya Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal inakamilika mwisho wa msimu huu. (Cadena Ser via Mirror)

Santi CazorlaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKandarasi ya Santi Cazorla Arsenal inakamilika mwisho wa msimu huu

Leicester City inatarajiwa kuwa klabu ya hivi karibuni ya ligi ya Premia kuingiza fedha zaidi katika kikosi chao cha wanawake kwa lengo la kupanda daraja katika ligi ya mabingwa - ikiwa ndio ligi ya daraja la pili ya wanawake. (Times - subscription required)
Maafisa wakuu wa klabu ya Real Madrid wamekataa ofa ya klabu hiyo kucheza mechi zake sita za nyumbani katika uwanja wa Wanda Metropolitano - Uwanja wa wapinzani wao Atletico Madrid. Uwanja wa Real-Santiago Bernabeu kwa sasa unafanyiwa ukarabati. (Marca)
Aliyekuwa mkufunzi wa Newcastle Steve McClaren amewaonya mashabiki wa klabu hiyo kutofanyia maamuzi wamiliki wapya wa klabu hiyo hadi pale watakapoanza kuisimamia klabu hiyo. (Talksport)

Post a Comment

0 Comments