tangazo

Tetesi za soka Ulaya Ijumaa tarehe 05.06.2020: Chilwell, Werner, Vertonghen, Longstaff

England Ben Chilwell anashawishiwa na kujiunga na Chelsea
Beki wa kushoto wa England Ben Chilwell 23, anashawishiwa na kujiunga na Chelsea baadae msimu huu lakini bado hajaomba kuondoka Leicester City . (Mirror)
Liverpool haitapambana na Chelsea kwa ajili ya kupata sahihi ya Timo Werner wakati mshambuliaji huyo,24, anayekipiga RB Leipzig yuko kwenye mpango wa kuelekea Stamford Bridge. (Evening Standard)
Tottenham wanamsubiri mchezaji wa nafasi ya ulinzi, Jan Vertonghen aamue juu ya hatma yake kikosiniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTottenham wanamsubiri mchezaji wa nafasi ya ulinzi, Jan Vertonghen aamue juu ya hatma yake kikosini
Tottenham wanamsubiri mchezaji wa nafasi ya ulinzi, Jan Vertonghen,33, kuamua kama ataendelea kubaki mpaka msimu utakapomalizika au ataondoka kabla msimu kuisha (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Newcastle Matty Longstaff hajakuwa mazoezini wiki hii wakati kukiwa hakuna uhakika kuhusu mustakabali wake kwenye klabu hiyo, huku klabu ya Udinese ya Serie A ikiripotiwa kutoa ofay a mshahara wa pauni 30,000 kwa wiki kwa mchezaji huyo, 20, ambaye mkataba wake utakwisha msimu huu. (Mail)
Manchester United wanajiandaa kumchukua kiungo wa safu ya ulinzi Brandon Williams
Image captionManchester United wanajiandaa kumchukua kiungo wa safu ya ulinzi Brandon Williams
Manchester City wanatarajia kuanza mazungumzo na mchezaji wa nafasi ya ulinzi Mhispania Eric Garcia huku klabu yake ya zamani Barcelona ikimtaka mchezaji huyo. (Mail)
Manchester United wanajiandaa kutoa mkataba mpya kwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi Brandon Williams ukiwa na marekebisho katika mshahara wake wa sasa wa pauni 40,000 kwa wiki, baada ya kufanya kazi nzuri msimu huu. (Athletic)
Arsenal wanaweza kuwa tayari kumuuza mchezaji wa nafasi ya ulinzi Kieran TierneyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionArsenal wanaweza kuwa tayari kumuuza mchezaji wa nafasi ya ulinzi Kieran Tierney
Arsenal wanaweza kuwa tayari kumuuza mchezaji wa nafasi ya ulinzi Kieran Tierney,23, kwa Leicester City, miezi 12 tu baada ya kuhamia Emirate(Express)
Kocha wa England Gareth Southgate hatahudhuria michezo ya ligi ya primia msimu utakapoanza kwa kuwa anahisi kuwa uwepo wake kwenye viwanja hauna umuhimu. (Star)

Tetesi bora Alhamisi

Jadon Sancho
Image captionReal Madrid wanapendelea kumsajili Jadon Sancho
Real Madrid wanapendelea kumsajili winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho,20. (AS)
Juventus imewasiliana na Barcelona kwa lengo la kusaini mkataba na mshambuliaji Mfaransa Ousmane Dembele, mwenye umri wa miaka 23, kwa mkopo msimu huu. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Ousmane Dembele huenda akaenda Juventus
Image captionOusmane Dembele huenda akaenda Juventus
Matumaini ya kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kuongeza kitita kwa ajili ya uhamisho kupitia mauzo ya wachezaji kama Marcos Roho, 30 , Beki wa kati Chris Smalling na mshambuliaji Alex Sanchez, 31, watakumbwa na athari zilizotokana na janga la virusi vya corona (Evening Standard
Ryan Fraser wa Bournemouth anayejiandaa kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu, anaweza kuwa mmoja kati ya wachezaji wanaohitajika sana kwenye ligi. (The Athletic)
Kocha Ole Gunnar Solskjaer atalazimika kuongeza kitita cha pesa kuwapata wachezaji anaowataka
Image captionKocha Ole Gunnar Solskjaer atalazimika kuongeza kitita cha pesa kuwapata wachezaji anaowataka
Paris St-Germain wanahitaji pauni milioni 156 kutoka Barcelona kwa ajili ya mshambuliaji wa Kibrazil Neymar, 28. (Sport in Spanish)
Watazamaji watakuwa na nafasi ya kusikiliza kelele za kutengeneza za mashabiki wakati Ligi ya Primia itakaporejea. (Mirror)
Kocha msaidizi wa Atletico Madrid, Burgos, 51 amethibitisha kuwa ataachia ngazi katika nafasi hiyo mwishoni mwa msimu huu na kuendelea na kazi kama kocha mkuu. (Marca)
Barcelona watatakiwa kutoboka mfuko kumpata NeymarHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBarcelona watatakiwa kutoboka mfuko kumpata Neymar
Barcelona ina mpango wa kumsaini tena beki wa kati wa Kihispania Eric Garcia,19, kutoka Manchester City. (ESPN)
Arsenal wako tayari kumpatia mchezaji wa nafasi ya ulinzi David Luiz,Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionArsenal wako tayari kumpatia mchezaji wa nafasi ya ulinzi David Luiz,
Arsenal wako tayari kumpatia mchezaji wa nafasi ya ulinzi David Luiz, 33, mkataba wa mwaka mmoja lakini watapunguza mshahara wake wa wiki (Mirror)
Manchester United wamebainisha kuwa winga wa Velez Sarsfield Thiago Almada,19, anawezekana akawa sehemu ya mpango wao wa uhamisho mbadala wa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 20. (Manchester Evening New

Post a Comment

0 Comments