tangazo

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 10.06.2020: Sancho, Havertz, Aubameyang, James, Thiago Silva, Hojbjerg

Chelsea inaamini kwamba mshambuliaji wa Borussia Dortmund na England Jadon sancho, 20, atajiunga na Man United
Chelsea inaamini kwamba mshambuliaji wa Borussia Dortmund na England Jadon sancho, 20, atajiunga na Man United hivyobasi inamnyatia kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz. (ESPN)
The Blues wamewasiliana na klabu ya Bundesliga ya Ujerumani kuhusu kumsaini Haverts mwenye umri wa miaka 20 , huku winga wa Brentford Said Benrahma akiwa katika orodha ya Chelsea. (Guardian)
Aston Villa wamekuwa wakivutiwa kwa muda mrefu na mchezaji wa Algeria Benrahma mwenye umri wa miaka 24 na watajaribu kumsajili iwapo wataepuka kushushwa katika ligi ya Premia. (The Athletic)
Beki wa kati wa Brazil Thiago Silva anataka kusalia barani Ulaya baada ya kuambiwa kwamba kandarasi yake katika klabu ya PSG haitaongezwa , na anaamini anaweza kuichezea timu kubwa kwa misimu miwili zaidi. (ESPN)
Thiago SilvaHaki miliki ya pichaEMPICS
Image captionBeki wa kati wa Brazil Thiago Silva anataka kusalia barani Ulaya
Klabu tano za ligi ya Premia - Arsenal, Everton, Newcastle, West Ham na Wolves - zinafikiria kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 kutoka PSG. (90 Minutes)
Arsenal ina matumaini kwamba uhusiano wake na babake mshambuliaji wa klabu hiyo Pierre-Emerick Aubameyang - ambaye ndiye ajenti wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 - atawasaidia kuandikisha kandarasi mpya na nahodha huyo wa Arsenal . (Telegraph)
Leicester City inamlenga beki wa kushoto wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico, 27, kuchukua nafasi yake mchezaji wa England Ben Chilwell, ambaye anahusishwa na uhamisho wa Chelsea na Manchester City. (Mirror)
Pierre-Emerick AubameyangHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionArsenal ina wanamatumaini baba yake Pierre-Emerick Aubameyang atawasaidia kuandikisha kandarasi mpya
Manchester United haiko tayari kumuachilia winga wa Wales Daniel James, 22, kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo - iwapo watamsaini mchezaji wa England Jadon Sancho. (Manchester Evening News)
RB Leipzig iko tayari kumuuza beki wa Ufaransa Dayot Upamecano,21 ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal, badala ya kumpoteza katika uhamisho wa bila malipo wakati kandarasi yake itakapokuwa ikikamilika Juni 2021. (Bild)
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Idrissa Gueye anasema hana lengo la kuondoka katika klabu hiyo licha ya mabingwa hao wa Ufaransa kumfungulia mlango wa kuondoka mchezaji huyo wa senegal mwenye umri wa miaka 30. Amehusishwa na uhamisho wa kurudi katika ligi ya Premia huku klabu za Wolves na klabu yake ya zamani Everton zikimtaka. (Le10Sport)
Idrissa GueyeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKiungo wa kati wa Paris St-Germain Idrissa Gueye hana lengo la kuondoka katika klabu hiyo
klabu ya Southampton huenda isikubali chini ya £35m ili kumuuza mchezaji Pierre-Emile Hojbjerg. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 raia wa Denmark analengwa na klabu za Everton na Tottenham. (Evening Standard)
Mabingwa wa Uhispania Barcelona wamepatiwa hadi tarehe 7 mwezi Julai kulipa Yuro 110m (£98m) ili kumruhusu mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez kuondoka katika klabu hiyo kabla ya kifungu hicho kupitwa na wakati. (Sky Sports)

Post a Comment

0 Comments