tangazo

Trump atuma tena Video ya ubaguzi ya Rangi Twitter


Donald Trump awali alishutumiwa kwa ubaguzi wa rangi wakati wa muhula wake wa urais
Rais wa Marekani Donald Trump ametuma video mtandaoni inayoonyesha mmoja wa wafuasi wake akipaza sauti na kusema "nguvu ya wazungu".
Mfuasi wake huyo alikua miongoni mwa kikundi cha watu waliokua wakishiriki mkutano wa kampeni ya uchaguzi ya Bwana Trump katika makazi ya kustaafu yaliyoko Florida.
Picha hiyo ya video ilionyesha wafuasi na wapinzani wa rais wakilumbana na kutupiana matusi.
Bwana Trump amekanusha shutuma kwamba anataka kupata umaarufu kupitia hali ya wasi wasi iliyopo kutokana na ubaguzi wa rangi nchini humo . Msemaji wake anasema hakusikia maneno "white power" katika video
Katika ujjumbe huo wa twitter, ambao baadae ulifutwa, rais aliwashukuru aliowaita "watu wazuri wa Vijijini " - akimaanisha watu waliostaafu wanaoishi Kaskazini-magharibi mwa Orlando ambako mkutano huo wa kampeni ulifanyika . "Wenye itikadi kali za mrengo wa kushoto hawafanyi lolote Democrats wataangushwa . Mfisadi Joe amepigwa . Tuonane hivi karibuni !!!," aliandika.
Video hiyo iliyowekwa katika ujumbe wa ilimuonyesha mfuasi wa Trump aliwa katika uwanja wa gofu huku akipaza sauti na kusema "nguvu ya wazungu ". Alionekana kuwa alikua akimjibu muandamanaji mwenzake aliyemuita mbaguzi wa rangi na kutumia maneno yasiyo ya staha. Waandamanaji wengine wanaompinga Trump walipaza sauti wakisema ''Nazi'' na maneno mengine ya shutuma dhidi ya waliohudhuria mkutano wa kampeni ya Trump.
Screengrab from tweet
Tim Scott, ambaye ndiye mtu mweusi pekee katika bunge la seneti la Marekani katika chama cha Republican, alisema katika mahojiano na CNN Jumapili kuwa video hiyo ilikua ni "kosa" na akamuomba rais aiondoe kwenye ukurasa wake wa Twitter.
"Bila shaka video ile isingepaswa kushirikishwa tena na anapaswa kuiondoa'' , Bwana Scott aliiambia televisheni hiyo.
Msemaji wa ikulu ya White House Judd Deere amesema kuwa rais "hakusikia kauli moja iliyotolewa katika video " lakini aliona "uungaji mkono mkubwa kutoka kwa wengi wa wafuasi wake".
Waziri wa Afya na Huduma za binadamu wa Marekani , Alex Azar, aliiambia CNN kwamba " Awe rais , utawala wake au mimi mwenyewe ninaweza kufanya chochote kupata uungajimkono wa wazungu ".
Rais Trump aliwali alikabiliwa na shutuma za kushirikisha na kunadi kauli za ubaguzi . Mwaka 2017 alituma video tatu za matusi kutoka kwa kikundi cha Uingereza cha mrengo wa kulia, na kusababisha aliyekua Waziri Mkuu wa uingereza wakati huo Theresa May kujibu.
Alikosolewa sana mwaka 2019 aliposema katika Twitter yake kwamba wajumbe wanne wanawake wa bunge la la Marekani - Alexandria Ocasio-Cortez, Rashida Tlaib, Ayanna Pressley na Ilhan Omar - wanapaswa " kurudi kutatua matatizo ya maene yaliyoharibika kabisa na yenye uhalifu mkubwa, ambako walitoka ". Watatu miongoni mwa wajumbe hao wa congresi walizaliwa nchini Marekani na wote wanne ni raia wa Marekani.
George Floyd
Maelezo ya picha,
Sita kati ya Wamarekani 10 wanapinga namna Trump alivyoshughulikia maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi yaliyoibuka baada ya kifo cha George Floyd
Akizungumzia maandamano ya wiki za hivi karibuni yaliyoibuka kutokana na kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd, Trump alionya kupitia twitter kuwa "wakati uporaji unaanza, ufyatuaji risasi unaanza " - kauli iliyotumiwa na mkuu wa polisi wa Miami Walter Headley alipokua akikabiliana na viguvugu la haki za kiraia mwaka 1967.
Kauli hiyo iliifanya kampuni ya Twitter kuondoa kauli hiyo kwa misingi kuwa imekiuka sheria za mtandao huo kwa kuchochea ghasia
Na Bwana Trump amekabiliwa na shutuma za ubaguzi wa rangi katika wiki za hivi karibuni kwa kutumia mara kwa mara neno "kung-flu" kuelezea virusi vya corona. Ikulu ya White House imekanusha kwamba matumizi ya neno hilo ni ubaguzi.
"Kile ambacho rais anakifanya ni kuelezea ukweli kwamba asili ya virusi ni China," alisema katibu wa masuala ya habari wa Ikulu ya White House Kayleigh McEnany.
Wakati huo huo, kura ya maoni ya kituo cha habario cha CBS News nchini Marekani inaonyesha kuwa wengi wa raia wa Marekani wanaafikiana na vuguvugu la watu weusi la Black Lives Matter na wanaamini kuwa maandamano yatawezesha kufanyika kamageuzi ya utendaji wa polisi nchini humo
Sita kati ya Wamarekani 10 wanapinga namna Trump alivyoshughulikia maandamano ya hijv karibuni ya kupinga ubaguzi wa rangi, kwa mujibu wa kura ya maoni, huku zaidi ya nusu yao wakisema ameshindwa kuonyesha uelewa wa kutosha juu ya sababu ya maandamano.

Post a Comment

0 Comments