tangazo

Ujerumani yaonya dhidi ya unyakuzi wa Israel.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Heiko Maas amesema Ulaya inapinga vikali mipango ya Israel ya kuanza kuyanyakua baadhi ya maeneo kwenye Ukingo wa Magharibi.


Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na waziri mwenzake wa Israel, Gabi Ashkenazi.
Ziara ya Maas mjini Jerusalem ambayo ni ya kwanza nje ya Ulaya tangu mripuko wa janga la virusi vya corona, inafanyika wiki chache tu kabla ya Israel kuanza kutanua himaya yake kwa kujenga makazi ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi, hii ikiwa ni kulingana na mpango tata kuhusu Mashariki ya Kati uliotangazwa na Rais Donald Trump wa Marekani.
Mpango huo ulikabiliwa na ukosoaji mkali kutoka kwa baadhi ya washirika wa karibu kabisa wa Israel, ikiwa ni pamoja na Ujerumani ambayo inasema marekabisho ya ramani ya Mashariki ya Kati yaliyofanywa na upande mmoja yanaweza kuvuruga matarajio yoyote ya kuanzisha taifa la Palestina na kufikiwa kwa makubaliano ya amani ya mataifa mawili.
Maas alisema kabla ya kuondoka Ujerumani kwamba "watu wengi nchini Israel na hata Umoja wa Ulaya bado wanatilia maanani hatua zilizopigwa katika mchakato wa kusaka amani ya Mashariki ya Kati pamoja na uwezekano wa mipango ya kuyanyakua maeneo hayo.

Post a Comment

0 Comments