Ujerumani yataka kuwa mpatanishi wa Marekani na China

Ujerumani inataka kufanya juhudi za upatanishi kati ya Marekani na China wakati wa muhula wake wa urais wa Baraza la Umoja wa Ulaya.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni, Heiko Maas ameviambia vyombo vya habari vya Ujerumani kuwa ulimwengu haupaswi kupasuka katika pande mbili za kimaslahi - upande wa China na upande wa Marekani.

Maas amesema Ujerumani itakumbana na changamoto wakati wa muhula wake wa miezi sita wa urais wa Umoja wa Ulaya, ambao utaanza Julai mosi.

Pia amesisitiza kuwa mkutano wa kilele unaopangwa kufanyika Septemba kati ya Umoja wa Ulaya na China utaendelea.

Mahusiano kati ya Marekani na China, ambayo tayari yalikuwa katika hali tete, yaliharibika hata zaidi wiki iliyopita, wakati Rais wa Marekani, Donald Trump alipotangaza hatua kuhusiana na sheria tata ya China ya usalama wa taifa kwa ajili ya Hong Kong.

Post a Comment

0 Comments