Umoja wa Ulaya utayari kuwa mwangalizi, uchaguzi Tanzania


Umoja wa Ulaya umesema upo tayari kuwa mwangalizi wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020 nchini Tanzania, endapo watapata ridhaa kutoka katika mamlaka husika.

Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa nchi za Afrika Mashariki Manfredo Fanti, amezungumza na wanahabari wa DW pamoja na Gazeti la East Afrika, ambapo mbali na mambo mengine aligusia suala la uchaguzi mkuu wa nchini Tanzania.

Tanzania ina jukumu la kuhakikisha uchaguzi huru

Balozi huyo amesema hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika baina ya taifa hilo la Afrika mashariki pamoja na jumuiya hizo ya kimataifa kuhusiana na suala la uchaguzi, ijapokuwa upo tayari kufanya uangalizi wa uchaguzi huo ambao utawaweka mamlakani, madiwani, wabunge na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Aidha balozi Fanti amesema taifa lina jukumu la kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi huru, haki na amani katika kipindi chote cha uchaguzi, huku akisisitiza kuwa umoja huo hauna mamalaka ya kuangalia uchaguzi bila mamalaka husika kutoa idhini.
Itakumbukwa kuwa sehemu ya kanuni za uchaguzi zinaeleza kuwa, Tume inaweza kutuma mwaliko kwa waangalizi wa kimataifa, jambo ambalo lilitoa wasiwasi kwa vyama vya siasa hasa upinzani kwamba huenda NEC isitoe fursa hiyo kwa jumuia za kimataifa kufuatilia kwa ukaribu zoezi hilo la kidemocrasia kama ilivyofanyika kwa chaguzi zilizopita.

Bofya Hapa Kusoma Habari Zingenezo

Post a Comment

0 Comments