tangazo

Umoja wa Ulaya wakosa mwafaka wa kufungua mipaka kwa wageniMataifa ya Umoja wa Ulaya jana yameshindwa kufikia makubaliano juu ya orodha ya nchi zilizo salama ambazo raia wake wangeweza kuruhusiwa kuanza kusafiri ndani na nje ya kanda hiyo kuanzia mwezi Julai.

Mabalozi wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya walikutana mjini Brussels jana kutayarisha mwongozo wa kuruhusu baadhi ya raia wa mataifa kadhaa duniani kuanza kuingia tena kwenye mataifa ya kanda hiyo bila ya masharti ya kukaa karantini.
Hata hivyo wanadiplomasia hao wameomba muda zaidi wa kushauriana na serikali za mataifa yao kabla ya kufikia uamuzi wa orodha ya nchi 10 hadi 20 zilizopendekezwa na uamuzi unatarajiwa kutolewa baadae hii leo.
Duru kutoka mjini Brussels zimesema orodha ya mataifa iliyowasilishwa kwa mabalozi hao haikuzujumuisha Marekani, Brazil wala Urusi, nchi ambazo bado zina kiwango kikubwa cha maambukizi ya virusi vya corona.
Kulingana na maafisa wawili wa Marekani abiria kutoka Marekani wataruhusiwa kusafiri ikiwa watatimiza masharti kadhaa ikiwemo kupita katika vituo vya ukaguzi wa joto la mwili.

Post a Comment

0 Comments