Virusi vya corona: Utegili wa wanaume una kiwango kikubwa cha kinga ya mwili

Wanaume ambao wamewahi kupata maambukizi ya virusi vya corona wanatakiwa kuchangia utegili wao (plasma) au majimaji yanayobaki kwenye damu baada ya kuondolewa kwa seli za damu ili uweze kutumika katika utafiti wa tiba ya ugonjwa wa Covid-19.
Utafiti unaonesha kuwa wanaume wako katika hatari ya kuwa wagonjwa zaidi na hivyo basi ndio wenye kiwango kikubwa cha kinga ya mwili kuliko wanawake.
Hii inamaanisha, plasma yaani utegili unaweza kuwa na umuhimu mkubwa kwenye kuokoa maisha ya walioambukizwa virusi vya corona.
Shirika la huduma za utoaji damu na viungo vya upandikizaji Uingereza limesema kuwa utegili unaweza kutumika kutibu wagonjwa wa corona walio hospitali ikiwa majaribio yanayoendelea yatafanikiwa.
Shirika hilo lilianza kuomba watu waliopona virusi vya corona kuchangia damu na utegili (plasma) kuanzia Aprili na kufikia katikati ya Mei, karibia watu 600 walikuwa wamechangia kwa kutoa utegili wao.
Wanaume waliochangia, asilimia 43 walikuwa na kiwango cha juu cha kinga ya mwili na kutumika katika majaribio, ikilinganishwa na asilimia 29 tu ya wanawake.
Kiwango cha juu cha kinga ya mwili mara nyingi kilikuwa ni kwa wagonjwa watu wazima, wagojwa wa Asia pamoja na wale ambao walishawahi kutibiwa ugonjwa wa virusi vya corona.
"Bado tungependa kusikia maoni ya yeyote ambaye alipata maambukizi ya virusi vya corona au kuwa na dalili za ugonjwa huo," Profesa David Roberts, kutoka shirika la uchangiaji damu na viungo Uingereza amesema.
"Watu wengi zaidi wanahitajika kuchangia utegili (plasma).
"Lakini hasa tungependa ikiwa wanaume wengi zaidi wangejitokeza."
Sio kila mmoja anaweza kuchangia majimaji yake ya kwenye damu (plasma).
'Kuchagia hakuchukui muda'

Simon na wazazi, Noel, wote waliathirika na virusi vya coronaHaki miliki ya pichaGARETH JONES

Simon Callon, 51, kutoka hospitali ya Helens, Merseyside, alichangia utegili wake baada ya kuanza kuugua virusi vya corona kisha akampoteza baba yake, Noel, kwa ugonjwa wa Covid-19.
"Haikuchukua muda," anasema, "na ni rahisi sana."
Simon hakuwa anakohoa wakati ameambukizwa lakini alikuwa anaumwa na kichwa kweli na kutetemeka usiku kwa siku kadhaa.
Alifanikiwa kupimwa kwasababu mchumba wake anafanyakazi katika wizara ya afya.
Wiki kadhaa baadae, baba yake alianza kuugua na kulazwa hospitali huku kiwango chake cha oksijeni kikiwa chini lakini hakupona.
"Sitaki mwengine yeyote apitie alichopitia baba yangu," Simon anasema.
"Alikufa hospitali bila familia wala rafiki zaidi ya wauguzi waliokuwa wamemshika mkono.
"Watu 10 ndio walioruhusiwa kuhudhuria mazishi yake.
"Unapoweza kumsaidia mtu au kunusuru maisha ya mwengine, msaidie."
Utegili (plasma) au majimaji ya damu ni nini?
Ni majimaji ya rangi ya njano ambayo huchangia karibia nusu ya idadi ya damu na yana seli nyekundu na nyeupe za damu na chembe za kugandisha damu (platelets) kote mwilini.
Baada ya mtu kuambikizwa virusi, utegili una kinga ya mwili inayotumika kukabiliana na maambukizi.
Kingamiwli yenye utegili inaundwa wakati mtu amepona maambukizi ya virusi vya corona, na kawaida huwa ni siku 28 baada ya kupona.
Kwanini ni muhimu?
Kinga mwili hii inaweza kupewa wagonjwa wa Covid-19 kwa kupitia mishipa kama ilivyo mtu anapotiwa damu kumsaidia kukabiliana na virusi vya corona na kuimarisha uwezo wa kupona.
Hospitali mbili Uingereza, kwasasa hivi zinafanya majaribio vile njia hii ya tiba inavyofanya kazi.
Aidha, majaribio mengine ya tiba kwa kutumia plasma yanaendelea nchini Marekani na kwengineko.
Je nani anayeweza kuchangia utegili huu unaohitajika kwa tiba ya corona?
Wale tu waliwahi kupata maambukizi au dalili za virusi vya corona na wamepona kabisa ili kutoa muda kwa kingamwili kujijenga.
Je hii ni sawa na kuchangia damu?
Ni tofauti.
Mchakato huu unachukua karibia dakika 45 na unatenganisha utegili (plasma) kutoka kwenye damu wakati unachangia.
Kawaida, mwili huzalisha utegili (plasma) nyengine kufidia zilizoondoka ndani ya saa 48.

Post a Comment

0 Comments