tangazo

WHO itaendelea kufanya kazi na Marekani

Shirika la afya ulimwenguni WHO limetangaza kuwa litafanyakazi pamoja na maafisa wa Marekani licha ya nchi hiyo kutangaza kujitoa kutoka katika shirika hilo.
Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema , kwamba michango na ukarimu wa serikali ya Marekani kwa shirika hilo la afya ulimwenguni katika miongo mingi, unatambulika sana kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya afya ya umma duniani kote.
 Rais wa Marekani Donald Trump Ijumaa iliyopita katikati ya janga la virusi vya corona alitangaza kusitisha uhusiano wa nchi yake na shirika hilo la afya ulimwenguni. Amesema kuwa shirika hilo linaunga mkono jinsi China ilivyoshughulikia udhibiti wa janga la corona.

Post a Comment

0 Comments