Tetesi za soka Ulaya Jumatano tarehe 01.07.2020: Sancho, Hojbjerg, Ake, Torres



Jadon Sancho hatagaraniwa zaidi ya pauni milioni 50
Manchester United haitalipa zaidi ya pauni milioni 50 kwa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho.
Hatahivyo, klabu hiyo ya Bundesliga inataka ongezeko la pauni milioni 100 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Sky Sports)

Arsenal wanafikiria kumtumia Matteo Guendouzi kama sehemu ya mpango wowote wa kubadilishana msimu huu

Maelezo ya picha,
Arsenal wanafikiria kumtumia Matteo Guendouzi kama sehemu ya mpango wowote wa kubadilishana msimu huu
Arsenal wanafikiria kumtumia kiungo wa kati Matteo Guendouzi, 21, kama sehemu ya mpango wowote wa kubadilishana msimu huu. (Mail)
Tottenham wanaamini kuwa watampata kiungo wa Southampton Pierre-Emile Hojbjerg,24, msimu huu lakini watapaswa kuwauza wachezaji kwanza. (Telegraph)

Manchester United wanafikiria kumchukua Nathan Ake

Maelezo ya picha,
Manchester United wanafikiria kumchukua Nathan Ake
Manchester City wana mpango wa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga katika klabu ya Bournemouth Nathan Ake, 25. Hatahivyo wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka Chelsea, ambao wanamtaka mchezaji huyo pia. (Athletic)
Beki wa kulia wa Barcelona Marc Jurado,16, ameondoka katika klabu ya Catalan. Mhispania huyo anajiandaa kujiunga na Manchester United msimu huu(ESPN)

Juventus wanamsaka winga Mhispania anayechezea Valencia, Ferran Torres

Maelezo ya picha,
Juventus wanamsaka winga Mhispania anayechezea Valencia, Ferran Torres
Juventus imeongeza ushawishi wao kwa winga Mhispania anayechezea Valencia Ferran Torres,20. Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Manchester United na Borussia Dortmund. ( Mail via Onda Cero)
Manchester City imekubali kumuuza winga Leroy Sane kwa Bayern Munich mchakato utakaowaingizia kiasi cha pauni milioni 54.

Manchester City imemuachilia Leroy Sane

Maelezo ya picha,
Manchester City imemuachilia Leroy Sane
Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Real Madrid Achraf Hakimi, 21,ameonekana Italia kabla ya uhamisho wa pauni milioni 36 kwenda Inter Milan. (Mail)
Roma imethibitisha kuwa mkopo wa Henrikh Mkhitaryan kutoka Arsenal umeongezwa mpaka mwishoni mwa msimu. Mchezaji huyo, 31, anayecheza nafasi ya kiungo wa kati alijiunga na timu hiyo ya Serie A mwezi Septemba. (Evening Standard)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Real Madrid Achraf Hakimi, 21,ameonekana Italia kabla ya uhamisho wa pauni milioni 36 kwenda Inter Milan

Maelezo ya picha,
Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Real Madrid Achraf Hakimi, 21,ameonekana Italia kabla ya uhamisho wa pauni milioni 36 kwenda Inter Milan
Manchester City imekamilisha mkataba wa kubadilishana wachezaji ambao utamuwezesha mshambuliaji, raia wa Uhispania Pablo Moreno mwenye umri wa miaka 18 kujiunga nao kutoka klabu ya Juventus, huku winga mreno Felix Correia, mwenye umri wa miaka 19, akielekea upande wa Serie A . (Guardian)
Mchezaji anayelengwa na Arsenal Layvin Kurzawa, 27, anatarajiwa kutia saini mkataba mpya wa miaka minne na klabu ya Paris St-Germain wakati kandarasi ya beki huyo wa kushoto wa Ufaransa itakapokamilika 30 June. (RMC Sport, via Sun)

Bofya Hapa kwa Habari Zingenezo.

Post a Comment

0 Comments