Ratiba Ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Kwa WILAYA YA MKURANGA



Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan,  Wana Mkuranga wapo tayari kwa kumpokea hapo Jumatano ya Tarehe 20/09/2023.


Mhe Rais anategemea kufanya ziara yake katika Kiwanda cha kutengeneza vioo kiitwacho SUPPHIRE FLOAT GLASS  kilichopo katika kijiji Cha Mkiu Kata ya Nyamato . Hiki ni kiwanda kikubwa zaidi Afrika mashariki na Kati chenye uwekezaji wa zaidi ya billion 700 

Mhe.Rais ataanza ziara yake kuanzia saa tatu kamili (3:00 asubuhi), Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan atafanya  mkutano wa hadhara na Wananchi wote wa Wilaya ya Mkuranga.


Aidha Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga  Mhe.Khadija Nassir Ally, anawataarifu na kuwaarika Wananchi wote wa Wilaya ya Mkuranga kumpokea Rais wetu  Kwa furaha, ndelemo na vifijo.

Hakika Taifa la Tanzania linaendelea mbele Kwa Kasi sana chini ya Rais Shupavu na Mahili , Dkt. Samia Suluhu Hassan

Post a Comment

0 Comments