Tetesi za Soka Ulaya Humate 18.09.2023

Scott McTominay

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kiungo wa Manchester United na Scotland Scott McTominay

Kiungo wa Manchester United na Scotland Scott McTominay, 26, ameibuka kuwa chaguo la Bayern Munich iwapo watamkosa Joao Palhinha wa Ureno, 28, kutoka Fulham mwezi Januari. (Mirror)

Ingekuwa ofa "ya kipuuzi" kwa Chelsea kufikiria kumuuza Reece James anayelengwa na Real Madrid kwa sababu beki huyo wa Uingereza, 23, yuko chini ya mkataba hadi 2028. (Football Insider)

Aston Villa wameungana na Liverpool na Barcelona katika mbio za kutafuta saini ya winga wa Athletic Bilbao mwenye umri wa miaka 21 Nico Williams, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao. (Diario AS - kwa Kihispania)


tt

Brighton wanatarajiwa kuwasilisha ofa mpya ya kumnunua beki wa Boca Juniors Muargentina Valentin Barco, 19, kabla ya dirisha la uhamisho la Januari. (Sun)

West Ham na Crystal Palace huenda wakafufua nia yao ya kumnunua mshambuliaji wa Paris St-Germain Mfaransa Hugo Ekitike, 21, mwezi Januari. (Football Insider)

Manchester United, Arsenal na Liverpool wanamfuatilia kiungo mshambuliaji wa Red Bull Salzburg mwenye umri wa miaka 19 Oscar Gloukh, ambaye sasa anaichezea Israel mara kwa mara. (Sun)

tt

CHANZO CHA PICHA,PARIS ST-GERMAIN

Mchezaji Conor Gallagher anayenyatiwa na Tottenham huenda akabadilisha msimamo wake kuhusu mustakabali wa klabu yake na kuamua kuondoka Chelsea ikiwa kiungo huyo wa Uingereza, 23, atapoteza nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza mara baada ya kupona jeraha. (Football Insider)

Winga wa Sunderland Muingereza Tom Watson mwenye umri wa miaka 17 amerejea kwenye darubini ya Nottingham Forest. (Sun)

Roma wanafikiria kuendelea na ombi la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata kutoka Atletico Madrid baada ya kufanya mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

tt

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata

Mshambuliaji wa Italia Ciro Immobile, 33, anatarajiwa kusalia na Lazio, licha ya kupokea ofa kutoka kwa klabu za Saudia za Al-Shabab na Al-Wehda. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

Kocha wa zamani wa Ujerumani Joachim Low ni miongoni mwa wagombea wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi ya Mjerumani mwenzake Stefan Kuntz kama kocha wa Uturuki. (DHA - kwa Kituruki)

Shirikisho la soka nchini Uturuki limeanza mazungumzo na mshambuliaji wa zamani wa Italia Vincenzo Montella, ambaye aliinoa Adana Demirspor ya Uturuki wa miaka miwili, kuhusu kurithi nafasi ya Kuntz. (Nicolo Schira)

Chanzo: BBC SWAHILI

Post a Comment

0 Comments