tangazo

Tanzania, ni nchi ya Uwazi, Taarifa zote kuhusu Corona Zinatolewa. Acheni uchochezi.

Virusi vya Corona: Maswali yaibuka juu ya uwazi wa taarifa za corona Tanzania

Maoni yangu katika jambo hili Mimi muandishi wa makala hii Joshua Vedasto. W, ninaamini serikali ya Tanzania inania njema kwa raia wake. Taarifa zote kuhusu Corona Zinatolewa vizuri Mara ya mwisho kulewa kwa Takwimu za Ugonjwa huu ilikua Jana Tarehe 29/04/2020. Hakuna haja yakufanya uchochezi katika jambo hili.

Naikumbukwe kwamba sio kila vifo vinavyotokea Tanzania vyote vinasababishwa na Corona!, hapana Bali vingine husababishwa na magonjwa mengine tuu.

Ushauri wangu kwa Raia wa Tanzania na Dunia, naomba tutambue kwamba uongozi wa awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuri unachapa kazi sawa sawa nahasa katika kupambana na gonjwa hili la Coronavirus.

Watu wote endeleeni kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu bila kulega lega, tusijifanye kuuzoea ugonjwa na kupuuza ushauri wa serikali na watu wa Afya.

MUNGU ibariki Tanzania, tutashinda tuu.

Post a Comment

0 Comments