Kim Jong-un: Ni nani anayeweza kuiongoza Korea Kaskazini bila Kim?

Uvumi kuhusu afya ya Kim Jong un huenda sio chochote, lakini maswali kuhusu mtu atakayemrithi katika kipindi cha muda mfupi ama mrefu yatakuwepo.
BBC ilkizungumza na wachanganuzi kuhusu walio na fursa ya kumrithi na iwapo historia itawakubali.
Mmoja wao ni mwanamume mmoja katika familia ya Kim ambaye amekuwa akiiongoza Korea kaskazini tangu ilipoanzishwa na Kim II sung 1984 na dhana kuhusu uongozi kutoka katika familia hiyo imekita mizizi katika jamii.
Propaganda kuhusu nguvu yake inaanza kwa raia kabla hata ya kuanza kusoma: watoto ambao hawajaenda shule huimba wimbo unaoitwa "Nataka kumuona kiongozi wetu Kim Jong-un."
Hivyobasi unawezaje kufikiria kuhusu Korea Kaskazini bila kiongozi huyo anayechukuliwa kama mfano wa kuigwa na mwanasiasa katika uongozini?
Je wasomi watajiandaa vipi pamoja na jamii?
Jibu la rahisi: hatujui, cha kuvutia zaidi ni kwamba pia nao hawajui. Hawajaweza kufanya hivyo.
Presentational grey line
Kim amekuwepo wakati wote ...
Archives: Kim Il Sung and Kim Jong Il in South Korea in November, 1994-Kim Il Sung and Kim Jong ll, Mt.Paekdu.Haki miliki ya pichaXINHUA
Image captionKim Il-sung ni muasisi wa Korea Kaskazini akiwa na mtoto wake Kim Jong-il aliyechukua mamlaka
Wakati Kim Jong-un alipokua akiandaliwa kuchukua mamlaka, walianza hata kutumia neno "kizazi cha Paektu " ili kusaidia kuhalalisha utawala wake.
Paektu ni mlima wa kusadikika ambako Kim Il-sung kana alianzisha vita vya msituni na ambako Kim Jong-il aliripotiwa kuzaliwa. Kim Jong-Un bado anaenda huko anapotaka kusisitizia maamuzi ya sera muhimu.
Wakati wote fikra za Kim zimekua zikifuatwa katika uongozi wa nchi.
Kim family tree
Image captionKizazi cha familia ya Kim
Je Korea Kaskazini itakuwaje bila kiongozi kama yeye? Kim Jong-un, 36, anaaminika kuwa na watoto - lakini bado ni wadogo. Inasemekana kwamba ana watoto watati mkuwa akiwa na umri wa miaka 10 na mdogo miaka 3. Kim Jong-un alisemekana kuwa bado nimdogo wakati anachukuwa madaraka akiwa na umri wa miaka 27.
Kuna uwezekano kukajitokeza kundi fulani la uongozi, pengine kama ilivyo kwa Vietnam, ambayo inayoegemea pakubw akwa mafundisho ya mwasisi wa taifa hilo.
Waangalizi wanaweza kfuatilia wale wanaoshikilia nyadhifa fulani na kufuata taarifa za kiintelijensia kuhusu taasisi muhimu lakini hawawezi kusema vile makundi kama hayo yanavyoendelea au nani yupo madarakani kwa sababu za kibinafsi wala sio kwwa ajili ya taasisi.
Aidha, wakati mwingine manaibu wanakuwa na nguvu zaidi madarakani kuliko viongozi wa taasisi. Na hilo linafanya iwe vigumu kutabiri chochote.
Kim watatu waliosalia
Kim Yo Jong, sister of North Korean leader Kim Jong Un, arrives at the opening ceremony of the PyeongChang 2018 Winter Olympic Games at PyeongChang Olympic Stadium on February 9, 2018 in Pyeongchang-gun, South Korea.Haki miliki ya pichaPATRICK SEMANSKY - POOL /GETTY IMAGES
Image captionKim Yo-jong, kama kiongozi pekee aliye katika ngazi ya juu yauongozi, ameibua matatarajio
Kuna Kim watatu ambao wanaweza kuwa wanahusishwa katika maamuzi ya nchi ya kisiasa iwapo -Kim Jonh-un atatoweka. Wote wanavikomo katika kuendelea utawala wa familia.
Wakwanza ni Kim Yo-jong, dada mdogo wa Kim Jong-un. Anasemekana kuwa ni mtu anayependelewa na baba yake ambaye aliwahi kuzungumzia uwezo wake, jinsi alivyopenda siasa tangu alipokua na umri mdogo. Tabia yake ni ya ufanisi, mwenye umakini kidogo, na anayeshuku na mchunguzi wa mambo.
Mengi yamefanywa ya kumfanya awe karibu zaidi na kaka yake.
Katika mkutano wa Singapore baina ya Trump na Kim alipata umaarufu kwa kumpatia kalamu kaka yake ya kusaini makubaliano na katika kikao kilichofuatia mjini Hanoi, alipigwa picha akionekana kwenye kona ya picha wakati kaka yake alipokua akipigwa picha kama za mkuu wa nchi.
Lakini ni mwanamke na hii inafanya liwe jambo gumu kuamini kuwa atachukua cheo cha juu katika jamii yenye mfumo dume uliokita mizizi.
Korea Kaskazini ni taifa la wanaume, ambalo jinsia ya mtu inaambatanishwa na matarajio.
Kuwa kiongozi wa ngazi ya juu, kuongoza jeshi, haifai katika sio kazi za mwanamke
Wapili ni Kim Jong-chul. Ni kaka mkubwa wa Kim Jong-un, lakini hakuwahi kuonekana kupendelea siasa au mamlaka.
Wamwisho ni Kim Pyong-il, kaka wa kambo wa Kim Jong-il . Mama wa kambo wa - Kim Jong-il - alitaka sana awe mrithi wa Kim Il-sung. Alishindwa na alitengwa na Kim Jong-il wakati ushawishi wake ulipopanda. Kim Pyong-il alipelekwa Ulaya mwaka 1979, ambako alichukua nyadhifa mbali mbali za kibalozi, akarejea Korea Kaskazini mwaka jana tu.
Hii inamaanisha kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba hana mahusiano mapana ya kumuwezesha kuwa miongoni mwa wanasiasa wasomi wa ndani wa Pyongyang.
Mtu wa pili mwenye mamlaka zaidi katika Korea Kaskazini kwa sasa.
Kama mjumbe maalumu wa Kim Jong-un Choe Ryong-hae (kulia) alikutana na viongozi wakuu wa mataifa ya kigeniHaki miliki ya pichaALEXANDER NEMENOV/AFP VIA GETTY IMAGES
Image captionKama mjumbe maalumu wa Kim Jong-un Choe Ryong-hae (kulia) alikutana na viongozi wakuu wa mataifa ya kigeni
Kuna watu wengine binafsi ambao wamekua watu wa ndani kisiasa katika enzi ya Kim Jong-un, lakini ni muhimu kufahamu ni nani miongoni mwao ataunda ushirika wa kifrafiki na ni nani atakayeshindana na mwingine.
Mmoja wao ni Choe Ryong-hae. Amekua na pandashuka zake chini ya Kim Jong-un, lakini kwa kuwa ameweza kupita dhoruba chache za kisiasa sasa ni makamu mwenyekiti wa kwanza wa tume ya masuala ya kitaifa. Mwaka jana alikua rais wa kwanzabaada ya miaka 20, akichukua nafasi ya Kim Yong-nam ambaye anazeeka - kwa hiyo ni mtu anayewakilisha Korea Kaskazini katika mazungumzo ya kimataifa.
Choe pia amewahi kushikilia nyadhifa katika jeshi na katika kitengo cha mipango na miongozo (OGD) cha chama cha wafanyakazi cha Korea, chenye jukumu la kuhakikisha kunakuwa na utiifu kwa utawala wakati wote. Shirika hilo lina mamlaka makubwa: huhakikisha raia wote wanafuata fikra ya Korea kaskazini. Huenda ni mtu wa pili mwenye mamlaka zaidi katika Korea Kaskazini.

Majasusi wa zamani na kuongezeka kwa mababu wa kisiasa

Kim Yong-chol alisafiri hadi Washington DC kukutana na Donald TrumpHaki miliki ya pichaOLIVIER DOULIERY-POOL/GETTY IMAGES
Image captionKim Yong-chol alisafiri hadi Washington DC kukutana na Donald Trump
Mwingine ni Kim Yong-chol. Jenerali huyu alitoa fursa ya kufanyika kwa mkutano kati ya Trump na Kim, ambapo alikutana na Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo mara kadhaa. Amekua Mkuu wa kitengo cha United Front (kinachohusika na mahusiano ya Korea Kaskazini )..
Mwingine tena ni Kim Jae-ryong. {amoja na kuwa katka tume ya masuala ya kitaifa , ni waziri maarufu katika baraza, ambaye ana ushawishi wa wastani. Ni machache yanayofahamiuka kumuhusu As well as being , lakini nyota yake imepanda katika kipindi cha miaka iliyopita huku wengine wakishuka. Anafahamika kama kwa kuongoza viwanda na kuongoza jimbo lililojitenga zaidi , ambako kuna viwanda vingi vya kijeshi, kwa miaka kadhaa. Hii inamaanisha kuwa amehusika kwa karibu katika mpango wa nyuklia.
Jong Kyong-taek anahusika na Idara ya tusalama ambayo huchunguza na kuadhibu uhalifu wa kisiasa. pia husaidia kuwalinda viongozi. huu ni wajibu muhimu ambao unasaidia kuimarisha uthabiti katika mfumo wa uongozi wa nchi.

Wanajeshi

Majenerali wachache wa ngazi ya juu wa jeshi la Watu wa korea -Korean People's Army (KPA) bila shaka watakua na ushawishi katika kipindi cha mpito .Kwasasa, wanaume wawili waliokalia viti vya juu katikataasisi kuu ya kisiasa nchini -General Political Bureau of the KPA, nao ni Kim Su-gil na Kim Won-hong. Tasisi hii inahusika na utekelezaji wa utiifu wa kisiasa katika jeshi , kitu ambacho kitakua muhimu bilashaka wakati wa kipindi cha mpito.
Kim Won-hong, husaidia kufafanua jinsi ilivyo vigumu kutabiri jinsi mamlaka yatakavyogawanywa iwapo Kim Jong-un hatakuwepo tena . Kim Won-hong na Hwang Pyong-s wamekuwa wakifikiriwa kuwa ni mahasimu, wakishindania kumshawishi Kim Jong-un kwa kuwatumia wengine.
Je miongoni mwa wasomi wakuu, ambao wanaweza kugongana na ni akina nani miongoni mwao watakua washirika? Je kutakua na mirengo ya wanaounga na wanaompinga -Kim Yo-jong? Je hofu ya kutoweka kwa uthabiti wa nchi itazuwia uadui wa kupita kiasi? Ni dhahiri kwamba wanasiasa wasomi hawataki kuona taifa likiporomoka, jambo ambalo linaweza kutoa fursa kwa ya kuchukuliwa na Korea kusini , au hata Uchina..
Kwasasa hakuna mgombea sahihi : dada yake atatakiwa kupita mtihani wa ubaguzi wa jinsia na kuvunja utamaduni wa urithi ambao kwa kawaida mrithi amekua ni mwanaume .Mtu mwingine yeyote hatatoka moja kwa moja katika kizazi cha damu muhimu cha Paektu. Lakini mwisho wa yote, watatakiwa kufikiria umoja wa taifa ambao wamekua wakiulinda.

Post a Comment

0 Comments