tangazo

UEFA yatarajia kuanza Ligi Mei 25


Ligi za kandanda barani Ulaya zimepewa hadi Mei 25 kulifahamisha shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA kuhusu mipango yao ya kuanza tena ligi za ndani.

Kandanda limesita kabisa katika ligi zote barani Ulaya na hakuna nchi iliyoanza tena ligi. Lakini UEFA inataka kuanza kupanga mashindano ya klabu ya Ulaya msimu ujao.

Katika barua kwa mashirikisho 55 yaliyo chini ya UEFA , rais wa shirikisho hilo Aleksander Ceferin aliandika kwamba ligi yoyote itakayofuta msimu wake itahitaji kutoa orodha ya timu ambazo zimefuzu kwa ajili ya mashindano ya klabu barani Ulaya.

Ceferin ameandika kuwa vyama vya kandanda vya kitaifa ama ligi vinapaswa kuwasiliana na UEFA ifikapo Mei 25 mwaka 2020 muda uliopangwa kuanza tena kwa ligi za ndani ikiwa ni pamoja na tarehe ya kuanza ligi hiyo na mfumo wa mashindano.

Post a Comment

0 Comments